Nuru FM

Mkurugenzi Mafinga Mji akabidhiwa ofisi

16 March 2024, 10:58 am

Ayoub Kambi kushoto akimkaribisha Mkurugenzi mpya wa Mafinga Mji. Picha na Hafidh Ally

Watumishi Mafinga Mji wametakiwa kushirikina na Mkurugenzi mpya wa Halmashauri hiyo hasa katika ukusanyaji wa mapato.

Na Hafidh Ally

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Itigi Ndugu, Ayoub Kambi amemkabidhi rasmi Ofisi Mkurugenzi wa Mji Mafinga Bi, Fidelica Myovela Hafla iliyofanyika katikati Ofisi ya Mkurugenzi na Kushuhudiwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Mafinga Mheshimiwa Regnant Kivinge.

Akizungumza wakati wa kukabidhi Ofisi hiyo Ayoub Kambi amewashukuru watumishi wa idara zote kwa ushirikiano waliouonesha hasa katika utoaji wa huduma za kijamii.

“ Ushirikiano Mkubwa nilioupata kipindi chote nipo Mafinga Mji ni Ushirikiano ambao nitauendeleza huko Itigi, tumesimamia Miradi ya Maendeleo bila kuchoka, tumesimamia ukusanyaji wa mapato yote hii ni kuhakikisha tunatoa huduma bora kwa wananchi, Hakika nimejifunza mengi Mafinga Mji” Ayoub KAMBI Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Itigi.

Baada ya kukabidhiwa Ofisi Mkurugenzi wa Mji Mafinga Bi, Fidelica Myovella amesema yupo tayari kufanya kazi na watumishi na kuwatumikia wananchi wa Mji Mafinga bila kuchoka kuhakikisha anaendeleza pale alipoishia Mkurugenzi Kambi.

“Uhai wa Halmashauri ni mapato, bila mapato hatuwezi kuwahudumia wananchi wetu hivyo lazima tuhakikishe tunakusanya ili wananchi tuwape huduma bora.
Pia ushirikiano mzuri baina ya watumishi na waheshimiwa Madiwani hufanya Halmashauri Kutulia, Naomba sana waheshimiwa madiwani ushirikiano wenu ili kusogeza mbele gurudumu hili la maendeleo la Halmashauri ya Mji Mafinga” Bi, Fidelica Myovella Mkurugenzi Mafinga Tc.

Kwa niaba ya waheshimiwa Madiwani Mwenyekiti wa Halmashauri Mheshimiwa Regnant Kivinge amesema imekuwa ni baraka kufanya kazi na Mkurugenzi Kambi Sasa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akaona atuletee Mwanamama Fidelica Myovella
“Tunakuhakikishia Ushirikiano Mkubwa na Karibu sana Mafinga”

Hafla hiyo ya makabidhiano imeshuhudiwa na Wakuu wa Divisheni na Vitengo wa Halmashauri ya Mji Mafinga kwa neno la shukrani na pongezi kutoka kwa Wakili Msomi Gasper Kalinga na Matida Yasin.