Nuru FM

Wanawake wenye Ulemavu Waiangukia Serikali

27 February 2023, 12:27 pm

Jukwaa la Wanawake wenye Ulemavu mkoa wa Iringa wakiwa katika ofisi ya kata ya Mkimbizi.Picha na Fabiola Bosco.

Kutokana na changamoto wanazokumbana nazo watoto wenye ulemavu wawapo shuleni.

Na Fabiola Bosco.

Baadhi ya wazazi wenye watoto walio na ulemavu wameiomba serikali kuwakumbuka kwa kuwapa usaidizi wa namna ya kuwahudumia Watoto wenye ulemavu wawapo shuleni pamoja na upande wa mikopo ya asilimia kumi.

Wakizungumza na nuru fm wamesema wamekuwa wakipitia changamoto mbalimbali pindi wanapowapeleka watoto shuleni kutokana upungufu wa walimu wenye uzoefu wa kuwahudumia watoto wenye ulemavu.

wazazi wa watoto wenye ulemavu wakieleza changaoto wanazokumbana nazo.

Kwa upande wake Afisa Elimu wa kata ya Isakalilo John Haruna amesema kuwa kila mtoto anahaki ya kupata elimu haijalishi ana upungufu gani hivyo ni vyema wazazi wenye watoto walio na ulemavu wakawasiliana na serikali za mitaa pindi fursa zinapotokea wakumbukwe zaidi.

Afisa Elimu wa kata ya Isakalilo John Haruna akiwataka wazazi kuchangamkia fursa zinapotokea.

Amesema kuwa utoaji wa taarifa unaweza pelekea wataalamu wakafika na kutambua ulemavu wa motto na kufahamu aina ya ulemavu alionao na shule anayopaswa kupelekwa kwa urahisi tofauti na kuwafungia ndani.

Afisa Elimu wa kata ya Isakalilo John Haruna akielezea umuhimu wa wazazi kutoa taarifa.

Kila mtoto ana haki ya kupata elimu na huduma za msingi kama binadamu wengine huku Ripoti iliyotolewa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu na Sayansi (UNESCO) ya mwaka 2000-2015 inaonesha watoto wenye ulemavu milioni 58 hawapo shuleni duniani na watoto milioni 100 hawamalizi shule.