Nuru FM

Viongozi wa Vyama vya Ushirika Mkoa wa iringa Wapigwa Msasa kusimamia Masuala ya fedha za Wanachama

1 April 2022, 3:29 pm

Jumla ya viongozi wa wapya wa vyama vya Ushirika wa akiba na Mikopo Mkoani Iringa 22 wamepewa mafunzo ya namna ya kuendesha vyama vyao katika ukumbi wa chuo kikuu cha ushirika Moshi Tawi la Iringa.

Akizungumza  mara baada ya kumalizika kwa mafunzo hayo yaliyoanza tarehe 29 mwezi wa tatu mpaka tarehe 1 mwezi nne, Mkufunzi kutoka chuo kikuu cha Ushirika Moshi Tawi la Iringa Bw. Godwin Majahasi amesema kuwa mafunzo hayo yalihusu viongozi wa bodi na kamati ya usimamizi juu ya usimamizi wa masuala ya fedha.

Amesema kuwa mafunzo hayo yamehusu, uongozi na utawala  bora katika bodi na kamati ya usimamizi, utunzaji wa kumbukumbu za uhasibu, na namna ya kusoma taarifa za fedha na namna ya kuzitafsiri.

Kwa upande wake Mrajiri msaidizi wa Vyama vya Ushirika Mkoa wa iringa Robert George amewataka viongozi hao kusimamia vyema maheshabu na kujuwa wajibu wao kwa kusimamia vyema mikopo iliyokopwa ili kuepukana na hati za mashaka.

Aisha amewataka viongozi hao kusimamia vyema majukumu yao na kuwa wabunifu kwa kuanzisha miradi ya kibiashara ambayo itasaidia vyama hivyo kukua na kuwa na mitaji mikubwa.

Awali Mwezeshaji wa mfunzo hayo Michael Mugolozi  amesema kuwa endapo viongozi hao watasimamia vyema aliyowandisha, vyama vitaweza kusimama imara kiuchumi na kuwanufaisha wanachama wake.

Nao baadhi ya washiriki wa Mafunzo hayo wakiwemo, Innocent Massawe kutoka Duka la ushirika la Iruwasa, Rehema abdala kutoka kilolo Saccos, Beatrice Mkakatu kutoka Saccos ya lulanzi na Chesco Chombo kutoka Mlandege Saccos wamesema kuwa mafunzo hayo yatakuwa chachu ya wao kuimarisha mifumo ya uongozi na ufuatiliaji wa taarifa za kifedha ili kukuza uendeshaji wa chama chao.

Mafunzo hayo ya siku nne yalianza tarehe 29 March mpaka tarehe 1 April yamefanyika katika ukumbi wa chuo cha ushirika Moshi tawi la iringa na yamelenga kuwapa mafunzo viongozi wapya Vyama vya ushirika waliochaguliwa katika Wilaya ya Kilolo na Manispaa ya Iringa.