Nuru FM

Mustafa Hamad awa mshindi wa kuhifadhi Quran juzuu 25 nyanda za juu kusini

17 April 2023, 1:40 pm

Kijana Mustafa Hamad akipokea zawadi ya loptop na Fedha Taslim katika mashindano ya kuhifadh Quran. Picha na Hafidh Ally

Mashindano ya kuhifadhi Quran Nyanda za juu kusini yalihusisha Mikoa ya Iringa Njombe na Dodoma kama Mgeni Mwalikwa huku vijana wakishindana kuanzia juzuu ya 1 mpaka ya 25 Iringa Mjini.

Na Hafidh Ally

Kijana Mustafa Hamad kutoka Madrasa ya DAR- Uloum Manispaa ya Iringa ameibuka mshindi wa kuhifadhi Quran Juzuu 25 katika mashindano ya Kuhifadhi Quran Nyanda za Juu kusini.

Akimtangaza Mshindi Huyo wa mashindano ya Kuhifadhi Quran yenye Kauli Mbiu TUUNGANE PAMOJA KUENDELEZA MAADILI, Jaji Mkuu wa mashindano hayo Shekh Omary Muhiya amesema kuwa mshindi huyo amepata alama 98 na atakabidhiwa shilingi Milioni Moja pamoja na loptop yenye thamani ya shilingi laki saba.

Wananchi wakifuatilia mashindano ya Quraan. Picha na Hafidh Ally

Kwa mujibu wa Jaji Muhiya mshindi wa pili wa juzuu 25 ni Bint Mgeni Salumu aliyejipatia shilingi laki 9 na Tv baada ya kupata alama 91.7 huku akiwapongeza vijana wote walioonesha umahiri wao kuhifadhi Quran.

Washindi wengine wa juzuu ya 1 ni Raniya Haruna, wa pili ni Nadya Mohamed, wa tatu ni Aisha Amiry, wa nne ni Murtadhwa Pandu na watano ni Sajda Upetee huku washindi wa Juzuu ya 2 wameongozwa na Hadya Abduljabar, Asma Chorobi, Taqiyu Mudathir, Nouriaty Mohamed na Swaleh Salum.
 

Washindi wa Juzuu ya 3 ni Swabri Salumu, Ramla Nasor, Hamad Bakar wakati washindi wa Juzuu ya 4 ni Abdulwahid Said, Salma Abdallah na Zakhiya Musa wakati walioshinda katika juzuu ya 5 ni Hajra Budy, Bin Yamin Musa na Baache Hamad.

Washindi wa kwanza katika mashindano ya Quran wakipiga Picha na Viongozi wa Dini na Serikali. Picha na Hafidh Ally

Aidha wahindi wa juzuu ya sita ni Haad Abduljabar, khalilu Abduljabdar na Shaffiih Gumbo huku walioshinda Juzuu ya 10 ni Mohamed Khalfan, Asiya Ramadhan na Shayma Shamsi, na katika juzuu ya 13 walioshinda ni Khamis Gumbo na Said Abdallah.

Washindi wengine ni Shabaan Ramadhn, Murshid Juma na Zainab abdallah katika juzuu ya 16 wakati walioshinda juzuu ya 22 ni Hadija Othman, Salmin Budy na Hassan Salimu.

Naye Mgeni Rasmi katika mashindano hayo Waziri wa mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Hamad Masauni ameahidi kuwachukua washindi wa nafasi ya kwanza kuanzia juzuu ya 16, 22 na 25 kuwapeleka Visiwani Zanzibar kwa ajili ya kushiriki tena mashindano ya Quran katika jimbo lake la Kikwajuni kwa gharama zake.