Nuru FM

PJT MMMAM yazinduliwa Iringa Manispaa

3 March 2024, 8:14 pm

Program Jumuishi ya Taifa ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto PJT-MMMAM ikizinduliwa katika Ukumbi wa Manispaa ya Iringa. Picha na Joyce Buganda.

Na Joyce Buganda

Mhe. Ibrahim Ngwada Mstahiki Meya Manispaa ya Iringa amezindua rasmi program jumuishi ya Taifa ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto PJT-MMMAM huku watendaji na wananchi wakitakiwa kushiriki vema katika kutekeleza programu hiyo.

Hayo yamezungumzwa na Mstahiki Meya wa Halmashauri ya manispaa ya Iringa Ibrahim Ngwada wakati akizindua programu hiyo na kusema kupitia serikali chini ya uongozi wa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan halmashauri imeendelea kuboresha huduma za mama na mtoto ikiwemo uimarishaji wa ujenzi wa miundombinu katika vituo vya afya, lakini pia katika nyanja ya elimu programu hii italeta tija na watoto wetu watakua vizuri ‘Alisema Ngwada.

GRACE SIMALENGA ni afisa maendeleo mkoa wa Iringa amesema programu hii ni nzuri kwani inamjenga mtoto kukua vizuri na kuujenga ubongo wa mtoto toka akiwa tumboni mwa mama yake hivyo watendaji wapeleke elimu hiyo mpaka kwenye ngazi ya kata ili wazazi na walezi waielewe vizuri programu hiyo.

PJT-MMMAM yenye lengo la kuchochea maendeleo ya awali ya mtoto katika kuhakikisha mtoto anafikia ukuaji timilifu, inamlenga mtoto mwenye umri 0-8 katika afua 5 ambazo ni AFYA, UJIFUNZAJI WA AWALI, MALEZI YENYE MWITIKIO, LISHE TOSHELEZI NA ULINZI NA USALAMA.