Nuru FM

Mbunge Nyamoga Aahidi ujenzi wa Shule ya Msingi

15 July 2023, 11:22 am

Mbunge wa Jimbo la Kilolo Mh. Justine Nyamoga Akizungumza na wakazi wa Kising’a jimboni Kwake.

Na Mwandishi wetu

Mbunge wa Jimbo la Kilolo, Mh Justine Nyamoga ameahidi kuanza ujenzi wa shule ya Msingi Kising’a ili kunusuru watoto wanaotembea umbali mrefu kufuata elimu.

Mh. Nyamoga ambaye yupo kwenye ziara inayolenga kusikiliza kero za wananchi wake katika Jimbo la Kilolo amesema ujenzi wa shule hiyo utaanza mara moja ili ifikapo January mwakani, wanafunzi waanze kusoma katika shule hiyo

Hata hivyo Nyamoga amewataka wananchi wa Kising’a kushiriki katika ujenzi wa shule hiyo ili iende kwa haraka na wanafunzi waanze kusoma mapema

“Niwaombe wananchi katika ujenzi wa shule hii kutakuwa na ajira nyingi sana sio vizuri wanakijiji wa kijiji kingine kuja kushiriki hapa naomba katika ujenzi wa shule hii kutakuwa na ajira naomba wanakijiji wa kata hii ndo muwe kipaumbele katika kupata ajira “ amesema Nyamoga