Nuru FM
Nuru FM
10 October 2024, 15:48

Na Adelphina Kutika
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imeahidi kuendelea kushirikiana na wafanyabiashara mkoa wa iringa ili kuboresha mazingira ya mazuri yatakayowawezesha kulipa kodi kwa wakati.
Hayo yamebainishwa na Kamishina mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Yusufu Mwenda katika kikao cha wafanyabiashara ,kilichofanyika katika ukumbi wa Royal Palm uliopo Manispaa ya Iringa ambapo amesema kuwa wataendelea kujenga mahusiano mazuri pamoja kusimia biashara zao ili kuchangia mapato ya Serikali.
Awali akiwasilisha taarifa ya Jumuiya ya Wafanyabiashara na TCCIA kwa Kamishina mkuu wa TRA,katibu mtendaji Kola Mtende wameomba serikali kupitia mamlaka ya mapato iwasaidie kupunguza utitili wa kodi hasa kwa wamili wa majengo.
Kwa upande wa wafanyabiashara, wameonyesha kuridhika na hatua hizo na wametoa mapendekezo kuhusu jinsi ya kuboresha huduma za TRA.
Hata hivyo Kikao hicho kimekuwa fursa nzuri ya kujenga mahusiano ya kudumu kati ya TRA na jamii ya wafanyabiashara.