Nuru FM

Mufindi waagizwa kujibu hoja za CAG

1 July 2026, 09:59

Mkuu wa Mkoa wa Iringa akiwa katika baraza la Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi. Picha na Fredrick Siwale

“Msipojipanga kujibu hoja za CAG Baraza la Madiwani linapaswa kuvunjwa”

Na Fredrick Siwale

Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Kheri James, ameizagiza Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi kujibu hoja za Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) katika mwaka wa fedha 2024/2025 ili kuongeza uwajibikaji na usimamizi mzuri.

Mh. Kheri ameyasema hayo wakati wa Baraza Maalumu la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi la kujadili Taarifa ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali, ambapo pamoja na kupata hati safi, halmashauri hiyo ilipitia hoja 64 zilizowasilishwa katika ripoti hiyo.

Mh. Kheri James amesema kuwa ni vyema baraza hilo likaweka utaratibu wa kukutana na wataalamu kueleza wanavyotekeleza majukumu yao kwani kutofanya hivyo kutapelekea baraza hilo kuvunjwa.

Sauti ya Kheri

Aidha Mh. Kheri James amewataka viongozi wa halmashauri kuendelea kuimarisha mifumo ya ukusaji wa mapato ili waweze kufikia lengo la kukusanya Bilion 10.3 katika mwaka wa fedha 2025/2026.

Sauti ya RC Kheri

Kwa upande wao, Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Dkt. Linda Salekwa, Mwenyekiti wa Halmashauri Castory Masangula, pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Mashaka Mfaume, wamemhakikishia Mkuu wa Mkoa kuwa watatekeleza maelekezo yote yaliyotolewa ili kuendelea kuboresha utendaji na kuimarisha maendeleo ya Wilaya ya Mufindi.

Sauti ya DC na Mwenyekiti

Hatua hiyo inalenga kuimarisha mifumo ya usimamizi wa fedha na kushughulikia kwa wakati hoja zilizobainishwa ili kudumisha uwazi, uwajibikaji na ufanisi katika utoaji wa huduma kwa wananchi.