Nuru FM

UVCCM Iringa yaanza maandalizi kuupokea Mwenge

11 May 2026, 08:57

Katibu wa Uhamiaji na Chipukizi UVCCM Mkoa wa Iringa Joseph Msigwa akizungumzai ujio wa Mwenge wa uhuru. Picha na Fredrick Siwale

“Ujio wa Mwenge wa Uhuru utasaidia kukagua miradi ya Maendeleo katika Wilaya ya Mufindi”

Na Fredrick Siwale

Umoja wa Vijana Chama cha Mapinduzi UVCCM Wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa umeanza kufanya Hamasa na maandalizi ya kuupokea Mwenge wa uhuru Mwaka huu 2026.

Akizungumza wakati wa ziara ya kukaguza maandalizi ya mwenge uhuru utakaofika Mkoani Iringa Kuanzaia May 26- May 30 mwaka huu, Katibu wa Uhamiaji na Chipukizi UVCCM Mkoa wa Iringa Joseph Msigwa amesema lengo ni kutembelea Vijana na makundi maalumu ili kufuatilia maandalizi Mbio za Mwenge wa Uhuru.

Sauti ya Msigwa

Msigwa amewataka amesema kuwa ujio wa mwenge wa Uhuru ni fursa kwa wananchi kujua miradi ya maendeleo inayotekelezwa na serikali sambamba na kurekebisha ile miradi ambayo bado haijakamilika kwa wakati.

Sauti ya Msigwa

Hivi Karibuni Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe.Kheri James aliongoza Kamati ya Ulinzi na  Usalama ya Mkoa na Wilaya katika Ziara ya kukagua Njia na Miradi mbalimbali inayotarajiwa kupitiwa na Mwenge wa Uhuru Mwaka 2026 ndani ya Halmashauri ya Mji Mafinga.

Mwenge wa Uhuru utapokelewa Mkoani Iringa  ukiongozwa na Kauli mbiu isemayo “Tanzania ni yetu sote,tushikamane kwa pamoja kuleta Maendeleo”.