Nuru FM

Chuo cha Rucu chawaandaa wahitimu kujiajiri

22 May 2026, 09:09

Mkurugenzi Mtendaji kutoka Kampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited Bw. Indrabhuwan Singh akiteta jambo na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Katoliki cha Ruaha (Rucu) Profesa Chrispina Lekule. Picha na Hafidh Ally

Tukio la Business Day limeonesha dhamira ya Chuo Kikuu Katoliki cha Ruaha (Rucu) ya kutoa elimu inayozalisha wahitimu wenye ushindani, ubunifu, maadili, na uwezo wa kufanya shughuli za kibiashara.

Na Hafidh Ally

Wanafunzi wa Chuo Kikuu Katoliki cha Ruaha (Rucu) Mkoani Iringa wametakiwa kutumia maarifa ya vitendo kupitia fursa za uwekezaji ili kujipatia maendeleo mara baada ya kuhitimu elimu ya Chuo.

Hayo yamezungumzwa na  Mkurugenzi Mtendaji kutoka Kampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited Bw. Indrabhuwan Singh ambaye alikuwa Mgeni Rasmi katika Tukio la Business Day lililowakutanisha wanafunzi wa Chuo cha Rucu kitivo cha Biashara, watumishi na wadau mbalimbali wa maendeleo ili kuwawezesha wanafunzi kupata maarifa wakati wakijiandaa kuishi maisha mara baada ya kumaliza elimu ya juu.

 Singh amesema kuwa fursa hiyo inaendana na matumizi ya teknolojia huku akiwataka wanafunzi hao kutokuogopa uwepo wa akili mnemba AI ambayo imeonekana kuwa kikwazo kwa vijana kupata ajira baada ya wanafunzi hao kuhoji uwepo wake ambao unaonekana kuwa kikwazo kwa vijana.

Sauti ya Singh

Naye Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Katoliki cha Ruaha (Rucu) Profesa Chrispina Lekule Amesema kuwa kupitia tukio hilo wanafunzi hao watajua siri ya kupata mafanikio kwa kutambua fursa mbalimbali zilizopo katika jamii.

Sauti ya Prof. Lekule

Naye Afisa Vijana Manispaa ya Iringa Bahati Mafungu ambaye alimwakilisha Afisa maendeleo ya Jamii Mkoa katika Tukio hilo amesema kuwa serikali inatambua uwepo wa vijana na wana wajibu wa kuhakikisha wanawaunganisha na wadau wa maendeleo ili kupata fursa za kujikwamua kiuchumi.

Sauti ya Bahati

Awali Rais wa Rucu Business Society Kitivo cha Biashara Chuo kikuu Katoliki Rucu Madaraka Romana Mmbinda amewashukuru wanafunzi wa Chuo hicho kitivo cha Biashara kwa kushirikiana kutekeleza tukio hilo ambalo limelenga kukuza uelewa masuala ya ujasiriamali na biashara.

Sauti ya Madaraka

Hata hivyo wanafunzi hao walipata Fursa ya kupewa elimu kutoka Taaisi ya uwekezaji UTT- ATMIS ya kuwaandaa vijana kuwa na maono ya biashara sambamba na kuwa na utaratibu wa kuweka akiba ili waweze kufanya uwekezaji kwa faida.