Iringa kufanya wiki ya utafiti na ubunifu
21 May 2026, 08:38

Wananchi Mkoani Iringa wanatarajia Kunufaika Na Maarifa Na Teknolojia Mpya kupitia maonesho hayo.
Na Hafidh Ally
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Kheri James, amewataka wananchi kutumia fursa ya Wiki ya Utafiti, Ubunifu na Huduma kwa Jamii kujifunza na kunufaika na tafiti mbalimbali zinazolenga kuimarisha maendeleo ya kiuchumi na kijamii.
Mh. Kheri amesema kuwa Maonesho hayo yanatarajiwa kufanyika kuanzia Juni 2 hadi 4, 2026 katika viwanja vya Bustani mjini Iringa, yakihusisha taasisi za utafiti, vyuo pamoja na wabunifu kutoka maeneo mbalimbali nchini.

Amesema kuwa kupitia Maanesho hayo wananchi watapata fursa ya kuona miradi mbalimbali iliyotekelezwa kutokana na utafiti uliofanywa na watafiti Mkoani Hapa.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Utafiti na Ubunifu wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa, Selina Mkimbili, amesema baadhi ya tafiti zitakazooneshwa zinahusu zao la ulanzi pamoja na uyoga unaozalishwa mkoani Iringa.

Tafiti hizo zinalenga kuongeza thamani ya mazao hayo pamoja na kuwasaidia wananchi kutumia mbinu bora za uzalishaji na uhifadhi ili kuongeza kipato na tija katika sekta ya kilimo.