Nuru FM

Mufindi waweka mkakati wa kuongeza ukusanyaji mapato

30 April 2026, 11:16

Mwenyekiti wa Hamashauri ya Wilaya ya Mufindi Mh. Masungula akiongoza kikao cha baraza la madiwani. Picha na Fredrick Siwale.

Mapato ya ndani Kwa Halmahsauri hiyo yameongezeka kutoka asilimia 41% hadi kufikia asilimia 52% katika robo ya tatu ya mwaka wa fedha 2025/26 , hali inayochochea kasi ya Maendeleo ya jamii.

Na Fredrick Siwale

Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi limeweka mikakati ya kuongeza ukusanyaji wa mapato ya ndani kwa kubuni vyanzo vipya vya mapato na kuimarisha ufanisi katika ukusanyaji wa ushuru.

Hayo yamezuzungumzwa katika kikao cha Baraza hilo katika ukumbi wa Itulavanu, Makao Makuu ya Wilaya ya Mufindi, na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Mh.Castory Masangula na kuongeza kuwa kuwa madiwani kwa kushirikiana na Mkurugenzi Mtendaji wanaendelea kuzitafutia ufumbuzi kwa wakati ili kuhakikisha mapato yanaendelea kuongezeka na kufikia malengo yaliyowekwa.

Sauti ya Masangula

Naye Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo ambaye pia ni Mwanasheria wa Halmashauri Ndg. Michael Haule amewataka watumishi na madiwani kuendelea kuwa wazalendo na kuongeza juhudi katika ukusanyaji wa mapato ya ndani, akisisitiza kuwa mapato hayo ni msingi wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa wananchi.

Sauti ya Kaimu Mkurugenzi

Kwa upande wao badhi ya madiwani wa Baraza hilo la Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi wameeleza kuwa wataendelea kusimamia kwa karibu utekelezaji wa mikakati hiyo mipya ili kuhakikisha mafanikio yanadumu na kuleta tija kwa maendeleo ya wilaya na ustawi wa wananchi kwa ujumla.

Sauti ya Madiwani