Nuru FM

CFS kuwanufaisha wakulima na wafugaji Iringa

30 April 2026, 10:49

Wanufaika wa Mradi wa CFS wakiwa katika Picha ya Pamoja. Picha na Joyce Buganda

Mradi huu umewasaidia wakulima na wafugaji kujua namna bora ya kufanya kilimo na ufugaji kisasa.

Na Joyce Buganda

Mradi wa mfumo wa mzunguko wa chakula (CFS) unaotekelezwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, hususan katika skimu za umwagiliaji za Kiwele na Magozi, umeanza kuonyesha matokeo chanya kwa wananchi wa maeneo hayo pamoja na jirani zake.

Akizungumza katika mkutano wa wadau wa kilimo uliowakutanisha wanufaika wa mradi huo wakiwemo wakulima na wafugaji, Profesa Mshiriki kutoka Chuo Kikuu Ardhi na mratibu wa mradi huo, Dkt. Makarius Mdemu, amesema mkutano huo umeandaliwa kwa lengo la kutathmini faida zilizopatikana kupitia mradi huo kwa wanufaika, pamoja na kujadili namna ya kuwafikia wananchi wengine ambao hawakunufaika katika awamu iliyopita.

Sauti ya Mdemu

Kwa upande wake, Afisa Maendeleo ya Jamii wa Wilaya ya Iringa, Saumu Kweka, ameishukuru CFS kwa kuichagua wilaya hiyo kutekeleza mradi huo, huku akiahidi ushirikiano wa karibu katika kuhakikisha makubaliano yaliyofikiwa yanatekelezwa kwa manufaa ya wakulima na wafugaji.

Sauti ya Kweka

Nao Baadhi ya wanufaika wa mradi huo wameeleza kuwa umechangia kwa kiasi kikubwa kuboresha shughuli zao za kilimo na ufugaji, hali iliyowawezesha kujikita zaidi katika kilimo biashara na kuongeza kipato chao.

Sauti ya wanufaika