Nuru FM

Mbunge Kabati aiomba Serikali kukarabati Barabara korofi Iringa.

17 April 2023, 4:41 pm

Mbunge akabati akichangia Hoja Bungeni katika Wizara ya TAMISEMI. Picha na Hafidh Ally

Wananchi wa Iringa wanashindwa kufanya shughuli za kiuchumi kutokana na ubovu wa miundombinu ya Barabara.

Na Hafidh Ally

Serikali imeombwa kukarabati barabara Korofi za Mkoani Iringa ambazo zimekuwa hazipiti katika kipindi cha Mvua ili kufungua shughuli za kiuchumi.

Hayo yamezungumzwa Bungeni Jijini Dodoma na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Iringa Mh. Ritta Kabati alipokuwa akitoa hoja katika Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais TAMISEM na kuongeza kuwa barabara nyingi zimekuwa ni changamoto na kupelekea shughuli za kiuchumi kusimama huku akiiomba serikali kupitia Tarula kukarabati barabara hizo.

Kabati ameongeza kuwa barabara ambzo zinahitaji kujengwa ni za Wilaya ya Iringa eneo la izazi-Mboliboli yenye urefu wa km 25, barabara ya Mtwivila-Ikongo yenye urefu wa km 1.5 huku Wilaya ya Mufindi kuna barabara ya Tambalang’ombe- kwa Mtenga Km 41, Luganga itimbo-isupilo yeye urefu wa Km 11.

Sauti ya Kabati

Kabati amebainisha kuwa katika Wilaya ya Kilolo kuna changamoto ya barabara za Mhanga- Mgeta km 18,  ilula- uhambingeto km 17, Mtandika- Nyanzwa km 40, Itimbo Kitelewasi KM 26, Ilula –Ibumu km 20 na barabara ya kitowo kwenda kisisiwe imekuwa na changamoto za muda mrefu.

Sauti Kabati

Akizungumzia katika Kada ya Afya, Mh. Kabati amebainisha kuwa Mkoa wa Iringa una upungufu wa watumishi wa afya zaidi ya elfu 2 huku akiiomba Wizara ya TAMISEM kuwapatia watumishi hao katika ajira mpya ambazo zimetangazwa na serikali hivi karibuni.

Sauti ya Mbunge

MWISHO