Nuru FM

Miradi ya fedha iwahusishe wananchi

28 February 2024, 8:56 am

Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Iringa Bashir Mhoja akizungumza kwenye kikao Cha baraza la Madiwani. Picha na Joyce Buganda

Na Joyce Buganda

Madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Iringa wametakiwa kushirikiana na watendaji kusimamia vizuri fedha za maendeleo zinazoletwa katika maeneo yao na serikali.

Akizungumza katika kikao cha baraza la madiwani Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Iringa Bashir Mhoja amesema kwa sasa mifumo imeshafunguka na fedha zimeshafikishwa kwenye Halmashauri hivo kinachotakiwa ni usimamizi mzuri wa fedha zitumike kwa matumizi yaliokusudiwa.

Mhoja amesema hapo awali mifumo ya fedha ilikuwa imefungwa kwaiyo ilikuwa inafanya miradi mingi kutokamilika kwa wakati kutokana na fedha kutotoka.

Mhoja ameongeza na kusema fedha nyingi zimekwisha ingizwa hivyo utekekezaji uanze mara moja pia kwa upande wa ujenzi wa shule kila darasa linagharimu milioni 25 mpaka kukamilika.

Aidha Mkuu wa Wilaya ya Iringa Veronika Kessy amewaomba madiwani kutoa taarifa pale wanapoona viashiria vya ubadhirifu na udokozi wa fedha ili miradi ikakamilike kwa muda” Tumepokea fedha nyingi za madarasa lakini pia washirikisheni wananchi ili fedha zinazobaki zikafanye maendeleo ya ziada katika sehemu ya mradi husika”Alisema Kessy lakini
undeni kamati katika maeneo yenu ili kuepuka sintofahamu za hapa na pale.

Steven Mhapa ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Iringa amesema madiwani na kamati ya fedha ya wilaya ya Iringa ipo vizuri kufuatilia mapato pamoja na kusimamia miradi lakini pia wanashukuru mifumo kufunguliwa ” mimi na madiwani wenzangu tumepokea maelekezo yote na tutayafanyia kazi.