Nuru FM

Mbunge Kabati aibana serikali kujenga kituo Cha afya Kimara Wilaya ya Kilolo

13 April 2023, 1:37 pm

Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Iringa Ritta Kabati akiuliza Swali Bungeni Jijini Dodoma. Picha na Hafidh Ally

Wananchi Kata ya Kimara Wilaya ya Kilolo wanakutana na changamoto ya kusafiri umbali mrefu kufuata huduma za afya kutokana na kutokuwepo kwa kituo Cha afya.

Na Hafidh Ally

Serikali imeombwa kujenga kituo cha afya katika Kata ya Kimara Wilaya ya Kilolo Mkoani Iringa ili wananchi waweze kupata huduma bora bora za afya.

Hayo yamezungumzwa bungeni Jijini Dodoma katika kipindi cha maswali na majibu wakati Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Iringa Dkt. Ritta Kabati alipouliza swali akitaka kujua ni lini serikali itawajengea kituo cha afya wakazi hao ambao wako pembezoni mwa wilaya ya kilolo.

Sauti ya Mbunge Kabati

‘Wananchi hao wamekuwa wakisafiri umbali mrefu kufuata huduma za afya katika kituo Cha afya Cha Dabaga’, Alisema Kabati.

Wananchi hao wamekuwa wakisafiri umbali mrefu kufuata huduma za afya katika kituo Cha afya Cha Dabaga, Alisema Kabati

Akijibu swali hilo Bungeni Jijini Dodoma Naibu waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mh. Festo Dugange amesema kuwa serikali imewasiliana na Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya kilolo kufanya tathmini ya kujua kata za kipaumbele ili kupeleka huduma za afya.

Sauti ya Naibu waziri Dugange

Amesema kuwa endapo Kata hiyo ni kipaumbele kwa halmashauri hiyo watawaandalia fedha kwa ajili ya ujenzi wa kituo Cha afya.

MWISHO