Nuru FM

Polisi Iringa wakabidhiwa pikipiki za kisasa 10

27 June 2023, 4:25 pm

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa ACP Allan Bukumbi akipokea Pikipiki 10. Picha na Adelphina Kutika.

Na Adelphina Kutika.

Jeshi la polisi mkoa wa Iringa limepokea msaada wa pikipiki 10 za kisasa zenye thamani ya shilingi milioni 55 na uzinduzi wa jengo la kantini yenye thamani ya shilingi milioni 45 kutoka kwa wadau mbalimbali wa maendeleo mkoani hapa.

Akizungumza katika halfa hiyo ya makabidhiano mkuu wa mkoa wa iringa bi Halima Dendego amewapongeza wadau kutoka sekta binafsi kwa kutoa vifaa vya usafiri kama sehemu ya kupanua wigo wa mapambano dhidi ya vitendo vya uhalifu pamoja na kurudisha fadhila kwa jamii.

Mkuu wa Mkoa wa Iringa Halima Dendego akiwa katika zoezi la kukabidhiwa pikipiki Jeshi la Polisi. Picha na Adelphina Kutika.

Kwa upande wao baadhi ya wadau waliofanikisha zoezi hilo ikiwa kampuni ya ASAS, EAST AFRICAN BORNWOOD , YISEN INTERNATIONAL INVESTMENT wakizungumza katika hafla hiyo wamesema kuwa lengo la kutoa mchango huo kutambua mchango wa kazi wanazofanya kwa wananchi.

Mstahiki meya wa halmashauri ya Manispaa ya Iringa IBRAHIMU NGWADA amesama kuwa taasisi nyingine zinapaswa kujifunza ili kuwatia moyo wadau wanaojitolea katika jamii.

Kamanda wa polisi mkoa wa Iringa ACP ALLAN BUKUMBI amesema kuwa kwasasa wanaendelea na zoezi la utoaji mafunzo kwa askali watakaotumia piki piki hizo ili kutambua matumizi sahihi na utunzaji wa vyombo hivyo.

Kantini ambayo itatumiwa na Polisi Mkoani Iringa.

MWISHO