Nuru FM

Yara kuibua tija ya kilimo Iringa

7 March 2024, 4:30 pm

Mkurugenzi wa kampuni ya Yara Winstone Odhiambo akizindua kituo Cha Mafunzo kwa wakulima wilaya ya Kilolo. Picha na Adelphina Kutika

Yara kuja na Mkakati wa kutoa mafunzo kwa wakulima yenye lengo la kuongeza usalishaji.

Na Adelphina Kutika

Kampuni ya Yara Tanzania imeanzisha kituo Cha Mafunzo ambacho kitakuwa kikihusika na kuibua tija ya wakulima na kuchangia kilimo endelevu kwa Mkoa wa Iringa

Kwa mujibu wa Mkurugenzi mkuu wa Yara Tanzania , Winstone Odhiambo alisema kuwa kituo hicho kwa Mafunzo kitawasaidia wakulima kukuza mbinu bora za kilimo ,kuboresha mavuno na kukuza kipato katika kaya .

” Kituo hiki Cha Mafunzo Cha Yara tunaamini baada ya muda fulani tutapata kukuza mbinu bora za kilimo kama vile afya ya udongo ,lishe bora ya mazao na kutunza mazingira kwa ajili ya uzalishaji endelevu wa chakula pia yatawawezesha wakulima kuboresha mavuno Yao na kurahisisha upatikanaji wa pembejeo za kilimo maarifa na mbinu za kilimo pamoja na matumizi ya ubunifu wa kidijitali lakini pia tutawawezesha wakulima wadogo ili kuongeza kipato Cha kaya na muktadha mzima wa kunufaika na utafiti wa maendeleo ,mnyororo wa thamani wa biashara ya kilimo na uvumbuzi ” Alisema Odhiambo

Alisema kituo Cha Iringa ni Moja ya vituo saba (7) ya Mafunzo vya Yara licha ya kuwa na vituo katika mikoa mbalimbali hapa nchini ukiwa ni pamoja na Mbeya Morogoro ,Kilimanjaro,Tabora ,Manyara na Zanzibar ambavyo vimekuwa vikikuza ushirikiano wa kimkakati na ukuaji wa kukuza mbolea na dawa za kuulia wadudu.

Yara inashirikiana na Farm for the future yenye makao yake Nchini Norway ya lengo la kuwakuza wakulima zaidi ya 2000 mpaka ifikapo mwaka 2030 kama ilivyo ndoto ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Osmund Ueland mwanzilishi wa Farm for the Future alisema amejifunza Mambo mbalimbali ndani ya mkoa wa Iringa kwani ndiyo sababu iliyompelekea kutowachukua wakulima kutoka nchini Norway akiamini ujuzi upo kwa wakulima waliopo .

Nimejifunza namna wakulima 2000 watakavyotabasamu Kweli ni Safari ndefu naamini Msingi kutoka Farm For the future utawasaidia wakulima kuondokana na umaskini na tumeamua kuondoka wenyewe hatutamsubiri yeyote nilileta fedha na ujuzi sijawahi leta wakulima kutoka Norway kwa sababu naamini Maarifa yapo hapa hii ni hatua kubwa na nitafuatilia ni nani atashirikiana nasi “Alisema Osmund

Katika hatua nyingine aliiomba serikali ili kurahisisha zoezi la utoaji wa elimu kwa wakulima kutekeleza Hadi yake ya kujenga visima vitatu kwa vijiji 16 zoezi ambalo litachochea kilimo Cha umwagiliaji .

Naye Mwakilishi wa Mkuu wa mkoa wa Iringa Mh.Peres Magir mkuu wa wilaya ya Kilolo alisema washirika watatu wa Yara Tanzania,Seed Co na Farm for the Future alisema zipo changamoto nyingi zinazowakabili wakulima katika mkoa wa Iringa ukiwa ni pamoja na ukosefu wa elimu ya kilimo ,pembejeo za kilimo kama vile mbolea miundombinu mibovu ,wadudu na magonjwa pamoja na teknolojia nafuu .

“Nimefurahishwa sana kwa kuanzishwa kwa kituo hiki Cha Mafunzo kunalenga kuyatuma changamoto mbalimbali zinazowakabili wakulima wetu hususan katika utoaji wa huduma za ugani ufumbuzi wa lishe ya mazao pamoja na kuwepo kwa changamoto mbalimbali zinazowakabili wakulima wetu hasa kwa ukanda huu wa wilaya ya Kilolo”Alisema Magiri

Clive Muganda ni Mkurugenzi mtendaji wa SeedCo . Aliyewakilishwa na Noel Shirima alisema kuwa SeedCo itaendelea kusaidia mpango wa kuendesha matumizi ya utafiti na ujuzi wa pamoja juu ya afya ya udongo na uendelevu wa Mazingira.

Muganda alipongeza ushirikiano wa Kampuni ya Yara Tanzania ,SeedCo na Farm for the Future huku akibainisha kuwa itawasaidia katika uhakika kwa wakulima kutokana na matumizi ya mbegu bora kutoka kwao .

SeedCo itaendelea kuongeza mnyororo wa thamani ya kilimo kwa ajili ya uzalishaji wa Mali shirikishi pia naamini kituo hiki kitaongeza ustahimilivu wa wakulima kwa sababu itachangia kupatikana kwa uhakika wa chakula na kukabiliana na umaskini miongoni mwa jamii za wakulima wadogo ” alisema Noel

Kwa upande wao baadhi ya wakulima wanaotoka katika vijiji mbalimbali Mkoani hapa walisema wanayashukuru mashirika hayo kwa yanawasaidia kuondokana na kilimo Cha kizamani ambacho kilifanya kupata mavuno machache licha ya kutumia Gharama kubwa na muda mrefu .

Walisema elimu hiyo itawasaidia kuondokana na umaskini kwani kwa kupata Elimu kutoka Farm for the Future,Mbolea nzuri kutoka Yara Tanzania na mbegu nzuri kutoka SeedCo itawasaidia kupata mavuno ya ndoto Yao .

Yara ni kampuni Tanzu inayomilikiwa na Yara international ASA ya Norway ikiunga maono ya ulimwengu usio na njaa na sayari inayofuata mkakati wa ukuaji endelevu wa thamani