Nuru FM

Vijana Iringa waaswa kugombea nafasi za uongozi

8 April 2024, 9:04 am

Mwenyekiti  wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Iringa, Elia Kidavile akizungumzia kuhusu vijana na uongozi. Picha na Adelphina Kutika

Kutojiamini, kukosa elimu ya uongozi, kukosa uzoefu, kutoaminika, kudharaulika ni miongoni mwa sababu zinazopelekea Vijana wengi washindwe kujitokeza kugombea nafasi za uongozi hapa nchini.

Na Adelphina Kutika

VIJANA Katika Halmashauri ya Wilaya Ya Iringa wametakiwa kujitokeza na kugombea katika uchaguzi unaotarajia kufanyika mwaka huu.

Wito huo umetolewa  na Mwenyekiti  wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Iringa, Elia Kidavile na kueleza kuwa  vijana wanapaswa kutambua wajibu wao katika kukisaidia chama hicho ili kushinda kwa kishindo.

Kidavile amewahimiza vijana kuepuka kutumika vibaya kisiasa na baadhi ya viongozi kwa maslahi yao binafsi, hasa katika kipindi hiki cha kujipanga kuelekea katika uchaguzi

Sambamba na hayo amesema umoja huo kupitia chama wamejipanga kudhibiti mianya ya rushwa ya ngono husasani kwa vijana wa kike watakaojitokeza kugombea nafasi yoyote ya uongozi.

MWISHO