Nuru FM

Sababu Za BM Kusaini Yanga Na Kuikacha Simba

4 July 2022, 3:44 pm

KIUNGO wa zamani wa Simba,Bernard Morrison ameweka wazi kuwa ambacho anakipenda na atakikumbuka kutoka kwa viongozi na mashabiki wa Simba ni upendo hivyo anaomba uendelee daima.

Kwa sasa kiungo huyo amerejea ndani ya Yanga aliyokuwa akiichezea zamani kabla ya kuwafunga Simba kwenye mchezo wa ligi kisha akasajiliwa ndani ya Simba.


Sababu kubwa ambayo imemfanya aweze kusaini Yanga ni pamoja na kile ambacho kinaelezwa kuwa kupunguziwa mshahara wake kwa asilimia kubwa jambo ambalo hakutaka liweze kutokea.

Pia ni moja ya kiongozi ndani ya Simba ambaye alikuwa akimlaumu mchezaji Morrison kwamba amekuwa hachezi kwa umakini kwenye mechi ambazo zinaihusu Yanga licha ya wakati mwingine kucheza akiwa anaumwa.

“Amekuwa akiambiwa kwamba hachezi kwa umakini kwenye mechi zinazoihusu Yanga jamo ambalo limepelekea aweze kutengwa na kuachwa hivyo hilo lilimpa hasira BM ambaye alikuwa anapendwa na kila mchezaji pamoja na mashabiki,”.

Usiku wa kuamkia Julai 4 Morrison ametambulishwa rasmi Yanga hivyo atakuwa ndani ya kikosi hicho msimu wa 2022/23.