Nuru FM

Ridhiwani aagiza watendaji waliojitolea Iringa kuajiriwa

22 November 2023, 8:06 am

Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akifafanua jambo.

Na Hafidh Ally

Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete amemwagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa kuwaajiri watendaji waliokuwa wakijitolea Katika nafasi zilizotangazwa hivi karibuni.

Mh. Kikwete ameyasema hayo baada ya Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Iringa Dkt Ritta Kabati kuuliza ni kwa nini watendaji waliokuwa wakijitolea kufanya kazi za utumishi hawakupewa kipaumbele wakati wa mchakato wa ajira Mpya Za Halmashauri zilizotangazwa na badala yake wakaajiriwa watumishi wapya.

Katika hoja ya Mh. Kabati Alisema kuwa Kitendo Cha kutowapa nafasi ya ajira vijana waliokuwa wakijitolea kitawavunja moyo Vijana wengine ambao wanafanya kazi ya kujitolea wakitegemea kuajiriwa pindi ajira zinapotangazwa.

Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Iringa Dkt Ritta Kabati

“Ukiangalia Katika Halmashauri yetu Kulikuwa na Vijana zaidi ya 40 waliopita kwenye usaili lakini waliojiriwa ni watendaji 10 Tena ambao wao Wana watu ambao wamewashika Mkono mpaka kupata nafasi hizo, ila wale ambao walikuwa wakijitolea na wana sifa zote wamekosa nafasi hizo, Naomba sana Mh. Naibu Waziri uliangalie hili” Alisema Mh Kabati

Akijibu hoja hizo Mh. Ridhiwan Kikwete Amemuagiza Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa kuwapigia simu vijana waliokuwa wakijitolea Katika nafasi hizo kabla ya Ijumaa na kuwapatia Ajira hao kwanza.

“Nikuagize Mkurugenzi uwatafute hao vijana ambao walikuwa na sifa ya kupata ajira waweze kuajiriwa kwa sababu walijitolea kwa moyo wakijua fika watapa ajira” Alisema Naibu Waziri Kikwete.