This image has an empty alt attribute; its file name is gg-1024x682.jpg
Nuru FM

Watendaji manispaa ya Iringa waagizwa kutatua kero za machinga

21 March 2024, 10:19 am

This image has an empty alt attribute; its file name is gg-1024x682.jpg
Mkuu wa mkoa wa Iringa Peter Serukamba akitoa maagizo kwa watendaji. Picha na Joyce Buganda.

Changamoto za machinga zinatakiwa kutatuliwa ili kukuza uchumi wa mkoa wa Iringa

Na Joyce Buganda

Watendaji wa halmashauri ya manispaa ya Iringa wameagizwa kushirikiana kutatua tatizo la machinga  ili kuleta maendeleo ya mkoa.

Agizo hilo amelitoa leo mkuu wa Mkoa wa Iringa Peter Serukamba wakati akimwapisha mkuu wa wilaya ya Kilolo na kuhimiza  viongozi wote washikamane usiku na mchana kufanya kazi za serikali ili kuuweka mkoa wa Iringa kwenye mstari ulionyooka.

Sauti ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa.

Joachim Nyingo ni mkuu wa wilaya mpya wa wilaya ya Kilolo amesema anamshukuru mhe. Rais kwa kumuamini na kumpeleka wilaya ya Kilolo na kuahidi kuitumikia wilaya hiyo kwa uadilifu.

Kwa niaba ya wananchi wa wilaya ya Kilolo mwnyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kilolo Ana Msola amesema viongozi na wananchi watahakikisha wanaendeleza ushirikiano  ili kuleta maendeleo .