Nuru FM

Kihenzile afuturisha, afanya dua ya kuliombea taifa

8 April 2024, 9:53 am

Mbunge wa Mufindi Kusini David kihenzile akiwa katika iftar aliyoandaa kwa wananchi wake. Picha na Mwandishi wetu.

Na Mwandishi wetu.

Mbunge wa Jimbo la Mufindi na Naibu Waziri wa Uchukuzi David Kihenzile ameungana na Viongozi wa Dini , Serikali pamoja na Wananchi kupata Iftar ya pamoja iliyoambatana na dua ya kumuombea Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa kuleta maendeleo katika kipindi cha miaka mitatu.

Iftari hiyo imefanyika nyumbani kwake kijiji cha Ibatu kata ya Igowole wilayani Mufindi mkoani Iringa.

Naibu Waziri Kihenzile amesema uamuzi huo wa kufanya dua ya kumuombea Rais Samia ni kwa sababu ya mambo mengi aliyoyafanya ikiwemo sekta ya elimu ambapo amesema tayari madarasa zaidi ya 30 katika Jimho hilo yameshaongezwa.

Aidha Kihenzile amebainisha kuwa katika Sekta ya barabara kukiwa na KM zaidi ya 30 ya barabara kutoka Luhunga hadi Ikani’ngombe na maeneo mengine korofi yameshakarabatiwa ambapo fedha nyingi zimetolewa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo ambayo ni ukombozi kwa Wananchi.