Nuru FM

Wakulima Iringa, Morogoro kunufaika na Mpango wa CCROs kutoka TAGRODE

5 January 2024, 7:26 am

Taarifa ya tathmini kuhusu mpango wa matumizi Bora ya ardhi. Picha na Adelphina Kutika.

Na Adelphina Kutika

Wakulima wadogowadogo na wafugaji kutoka vijiji vinne vya mikoa ya Iringa na Morogoro wanaenda kunufaika na mipango wa matumizi bora ya ardhi na hatimiliki za kilmila (CCROs) baada la Shirika la Tanzania Grassroots Oriented Development (TAGRODE) la mjini Iringa linalofanya miradi ya maendeleo mbalimbali, kutekeleza mradi wa majaribio wa kujengea uwezo jamii kutambua haki ya kumiliki na kulinda ardhi.

Hayo yalibanishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la TAGRODE, Bw Zubery Mwachulla wakati wa kikao cha tathmini yaani reflection meeting baada ya utetekelzaji wa mwaka moja wa mradi kilichofanyika katika Mji Mdogo wa Ilula wilayani Kilolo, mkoani Iringa hivi karibuni.

Alisema kuwa katika Mkoa wa Iringa mradi huo unafanya kazi kwenye wilaya za Kilolo na Iringa, ambayo katika Wilaya ya Kilolo ni katika Kijiji cha Ikula na Wilaya ya Iringa (Iringa DC) ni katika Kijiji cha Nyakavangala.

Bw Mwachulla
alibainishwa kwamba lengo kuu lilikuwa ni kuwajengea uwezo jamii za wakulima wadogo wadogo na wafugaji, ili kusaidia serikali za vijiji kusimamimia vizuri suala la utatuzi migogoro ya ardhi.

Aidha wananchi wanatakiwa kutambua wajibu wao, wa wakutengeza mpango wa matumizi bora ya ardhi (VLUP), ili waweze kuheshimu maeneo yaliotengwa, mfano, chanzo cha maji, badala ya watu kulima au kunywesha mifugo katika chanzo cha maji nakadhaliki.

“Kwa mwaka mmoja mradi ulilenga katika jamii ili iweze kuwajibika na vilevile kamati zao za masula ya ardhi ziweze kuwajibika ili kuleta maendeleo endelevu.

Sasa jambo kubwa tunaloliangalia vilevile ni suala la jinsia (wanawake, wanaume na vijana wakike na wakiume) waweza kupata haki sawa na mradi unalenga wakulima na wafugaji ili waweze kuzuia kiwango cha migogoro baina ya makundi hayo mawili,” alisema.

Mradi wa Ehancning Land Rights and Land Security of Rural Communities in Iringa and Morogoro regions, unafadhiliwa na Shirika la Bread for the World (Brot Fur die Welt) kutoka Ujerumani ambao ni mradi wa majaribio wa miaka mitatu (2023-2025), lakini ukifanya vizuri utapanuliwa katika maeneo mengine Zaidi, alifafanua Bw Mwachulla.

“Kwa mwaka moja wa utekelezaji wa mradi tumeweza kuwajengea uwezo, uelewa na kutoa elimu katika makundi hayo mawili (wakulima wadogo na wafugaji), kuhusu haki za ardhi, lakini pia kuwajengea uwezo serikali za vijii pamoja na kamati zao kuhusu uwajibikaji katika kutatua migogoro ya ardhi…,” alifafanua Bw Mwachulla.

Alisema kuwa katika tathmini hiyo picha kubwa iliyojitokeza ni kwamba wamefanya vizuri katika kuanzisha majukwaa ya jamii ya ardhi (Community Forum) ambayo ni ya vijana 20 kilia kijiji, yaani wanawake 10 na wanaume 10.

“Haya majukwaa ya jamii yamekuwa ngazi au daraja katika mradi na jamii, yaani kwa kutoa elimu kuhusu haki za kumiliki ardhi na kufanya ushawishi na utetezi ili serikali za vijiji ziweze kuwajibikia Zaidi…,” alisema.

Bw Mwachulla aliongeza kuwa serikali za vijiji zimeona majukwaa ya (CF) haya ni ya msingi katika kusaidia kuhamasisha na kupunguza migogoro ya mbalimbali katika maeneo yao.

Bw Francis Kivike ni Katibu wa Jukwaa la Jamii (CF) kutoka katika Kijiji cha Ikula Kata ya Ruahambuyuni, Tarafa ya Mahenge wilayani Kilolo, alisema jukwaa hilo limeweza kusaidia kupunguza migogoro mbalimbali ya viwanja na maeneo ya ardhi katika kijiji chao.

“Wananchi wamepatiwa elimu ya haki ardhi na kuwezakutatua changamoto ya mipaka ili wasiweze kutumia maeneo ambayo sio ya kwao,” alisema Bw Kivike.

Bw Kiviki alieleza kuwa kabla ya kuanzishwa kwa CF kijiji kilikuwa na hali sio nzuri katika umiliki wa ardhi, kwamba wananchi wengi walikuwa hawana uelewa wa kutosha juu ya umiliki wa ardhi na matumizi yake.

“Mmoja ya majukumu ya jukwaa la jamii ni kwamba wanapata mafunzo kutoka kwa wawezeshaji ili na sisi pia tutoe elimu kwa jamii, pamoja kupata mrejesho kutoka kwa jamii na kupeleka kwenye shirika,” alisema.

Katibu huyo alisema kuwa mpka sasa elimu inahitajika kutolewa na wananchi na wanaendelea kuipokea kwa mtazamo chanya, huku akiongeza kwamba kabla ya kuanzisha kwa jukwaa la jamii la ardhi hali ilikuwa sio nzuri katika umiliki wa ardhi.

Bi Kalista Maginge ni mwenykiti wa baraza la sheria la kata ya malengamakali, katika tarafa ya Isimani wilayani Iringa, alisema kuwa majukumu ya baraza hilo ni kutatua migogoro mchanganyiko ikiwemo migogoro ya ardhi nay a ndoa na mingine mingi.

Alisema kuwa ameshukuru mradi wa kujengea uwezo jamii kufika katika kijiji chao cha Nyakavangala ambao utasidia sana wanawake kupata hatimiliki pamoja na watoto wakike kupata ardhi.

“Hapo nyuma tulikuwa tunajua kwamba watoto wakike hawana haki ya kumiliki ardhi, lakini kutokana na elimu inayoendelea kutolewa tunajua kwamba tunahaki ya kumiliki hatimiliki ardhi za kimila (CCROs),” alisema Bi Maginge.

Hapo wali, Kijiji cha Nyakavangala kilikuwa na changamoto ya migogoro ya ardhi lakini kupitia elimu mbalimbali zinaendelea kutolewa mgogoro hiyo inazadi kupungua, alielezea.

“Wito wangu kwa kinamama wote wa Kiji cha Nyakavangala naomba tukusanyike kwenye mikutano iwe ya hadhara, mkutano mkuu wa kijiji, iwe mkutano wa taasisi tukusanyike ili tuweze kujua haki zetu za msingi katika kumiliki ardh…,” alisema Bi Maginge.

Kwa upande wake, Ofisa Mipango wa Miji na Vijiji wa Wilaya ya Kilolo Bw Bernard Kajembe, “sisi kama wilaya tunashirikiana na mashirika kama TAGRODE, ambao tunashirikiana nao katika masuala ya ardhi, hasa katika kuwaweza wananchi kwa kutoa elimu ili waweze kuondikana na migogoro ya ardhi,” alisema.

Alisema kuwa mashrika hayo yanasaidia kwa kiasi kikubwa, ambapo aliongeza kuwa hao kama halmashauri hawana funds (fedha) yakufika katika vijiji vyote kwa wakati mmoja.

Bw Kajembe alielezea kwamba kwa kushirikiana na mashirika wanaweza kufika vijiji vingi Zaidi kikiwemo kijiji cha Ikula kutoa elimu ya ardhi, sheria za ardhi na jinsi ya kutatua migogoro na kuleta tija kubwa katika halmashauri ya wilaya ya Kilolo.

“Kama Halmashauri ya Wilaya ya kilolo waendelea kutoa ushirikiano kwa asilimia mia ili kuweza kuwanufaisha wananchi wetu hasa wakati tunaenda kupima mashamba yao ili kupata hatimiliki za kimila (CCROs) ili ziweze kuwasaidia katika maisha ya kila siku,” alifafanua Bw Kajembe.

Hata hivyo katika Mkoa wa Morogoro mradi huo unatekelezwa katika halmashauri ya Mlimba vijiji vya Viwanja Stini na Ikule na Mlimba yenyewe .