Nuru FM

Wananchi washauriwa kukamilisha dozi ya chanjo ya Uviko-19

30 March 2023, 12:26 pm

Ni muhimu kwa jamii kupata dozi mbili za chanjo ya Uviko-19 ili kukabiliana na Maambukizi mapya ya Virusi vya Corona.

Na Ashura Godwin

Idara ya Afya mkoa wa Iringa imewataka wananchi kujitokeza katika vituo vya afya ili kupata na kukamilisha dozi ya uviko-19 itakayosaidia kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona.

Hayo yamezungumzwa na Mratibu wa chanjo mkoa wa iringa Hansi Mapunda amesema ni muhimu kwa jamii kupata dozi mbili huku akitaja aina ya chanjo ambazo zinatolewa mkoani hapa ambazo zinalenga kuongeza kinga.

Kwa upande wake Kaimu  Mganga mfawidhi  kutoka   hospital ya rufaa mkoa wa iringa DK. RIOKI MWITA amebainisha kuwa idara ya afya inaendelea na zoezi la  utoaji wa elimu kwa wananchi juu umuhimu wa kupatiwa chanjo ya ziada ya uviko19 maarufu kama booster ili kuendelea kujikinga na maambukizi mapya ya virusi hivyo.

Nao baadhi ya Wananchi Manispaa ya Iringa wamesema tayari wana elimu kuhusu chanjo za uvoko -19 jambo lililopelekea wasiwe na hofu kuhusu chanjo hiyo.

“Kwa kweli tunashukuru sana toka tumepewa elimu ya chanjo ya Uviko-19 imesaidia sisi kufanya maamuzi ya kuchanja” walisema

Dozi ya nyongeza ya COVID-19 maarufu kama Booster ni dozi ziada ya chanjo inayopewa angalau miezi 6 baada ya kozi ya kwanza ya chanjo 2 za COVID-19.