Nuru FM

Mafinga kupokea mwenge Juni 25

4 April 2024, 10:30 am

Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Dkt Linda Salekwa akiwa kwenye kikao Cha maandalizi ya mwenge. Picha na Hafidh Ally

Mwenge wa uhuru ni mojawapo ya alama za kitaifa za Tanzania ambao huzunguka kila mkoa kwa lengo la kuangalia maendeleo ya miradi mbalimbali ya maendeleo katika jamii.

Na Hafidh Ally

Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mheshimiwa Dkt. Linda Salekwa ameitisha kikao cha kwanza cha Maandalizi ya Mbio za Mwenge 2024 ambapo Mkoa wa Iringa unategemea kupokea Mwenge wa Uhuru 2024 Tarehe 22/6/2024 na Wilaya ya Mufindi inategemea kupokea Mwenge kutoka Njombe.

Halmashauri ya Mji Mafinga inategemea kupokea Mwenge tarehe 25/6/2024 na utakabidhiwa tarehe 26/6/2024 katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa.

Aidha Mkuu wa Wilaya amezitaka Halmashauri zote Mbili za Wilaya ya Mufindi kuhakikisha Miradi iliyopendekezwa ikamilike Kama haijakamilika na taarifa za Miradi yote zipitiwe na kukaguliwa kabla ya Mwenge Kufika.

Dkt Linda Salekwa amewataka Wakuu wa Taasisi zote, Wananchi na Watumishi kuhakikisha wanafanya Maandalizi ya kuupokea Mwenge wa Uhuru 2024 sehemu zote utakapopita kwani Mwenge unaleta na kuchachua Maendeleo ikiwa ni pamoja na kukamilisha Miradi, kufichua wala rushwa na kusambaza jumbe mbalimbali za Kitaifana.

Akitoa taarifa ya Halmashauri ya Mji Mafinga kwa Niaba ya Mkurugenzi wa Mji, Mratibu wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Mji Mafinga Ndugu Henry Kapella amesema Mwenge Utakesha katika uwanja wa Mashujaa Katikati ya Mji wa Mafinga.