Nuru FM

Diwani Nziku awahimiza wanawake Iringa kutunza Mazingira

3 March 2025, 11:03

Diwani Dorah Nziku akipanda Mti. Picha na Halfan Akida

Na Halfan Akida

Wanawake wa Manispaa ya Iringa wamehamasishwa kuwa na utamaduni wa kutunza mazingira ikiwemo kupanda miti ya vivuli pamoja na matunda katika maeneo yao.

Wito huo umetolewa na , Diwani wa Viti maalum Manispaa ya Iringa, Dora Nziku katika uzinduzi wa wiki ya Maadhimisho ya siku ya Mwanamke Duniani ambapo wanawake wa manispaa ya Iringa wameshiriki uzinduzi huo kwa kupanda miti 150 katika shule ya Sekondari ya Kwivava iliyopo Kitwiru ili kuondokana na athari za mabadiliko ya tabia ya Nchi.

Sauti ya Nziku

Amesema Upandaji wa miti utasaidia kupunguza kiwango cha joto Duniani pamoja na kukosekana kwa mvua kunakohatarisha hali ya upatikanaji wa chakula.

Sauti ya Nziku

Kwa upande wake, Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Manispaa ya Iringa Tumo Dosi amewaomba wanawake kujitokeza kushiriki kongamano la siku ya Wanawake Duniani ili kuzifahamu fursa mbalimbali zinazotolewa na serikali.

Sauti ya Dosi

Uzinduzi wa wiki ya Wanawake utaenda sambamba kwa kufanya shughuli mbalimbali ikiwemo utoaji wa elimu ya masuala ya Ukatili wa Kijinsia.

MWISHO