Nuru FM

Serikali yakabidhi magari kusaidia mradi wa TACTICS Iringa

11 August 2026, 18:16

Mradi huo unatekeleza miradi mikubwa mitatu yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 20, inayohusisha ujenzi wa soko, barabara pamoja na Jengo la Mhandisi, kwa lengo la kuboresha miundombinu na huduma za kijamii katika Manispaa ya Iringa.

Na Hafidh Ally

Serikali imekabidhi magari mawili yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 200 kwa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa, kwa ajili ya kusaidia utekelezaji wa Mradi wa Kuboresha Miji 45, TACTICS.

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Benjamin Sitta, amesema TACTICS ni miongoni mwa miradi muhimu inayoonesha dhamira ya Serikali ya kuleta mageuzi katika miundombinu ya miji.

Sauti ya DC Sitta

Aidha, Sitta amewataka watumishi wanaotekeleza mradi huo kuyatunza magari hayo ili yaendelee kuwa na matumizi katika shughuli nyingine za Serikali baada ya kukamilika kwa miradi ya TACTICS.

Sauti ya DC Sitta

Kwa upande wake, Mhandisi wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa, Rajabu Msangi, amesema magari hayo yataongeza ufanisi katika usimamizi, ufuatiliaji na utekelezaji wa miradi mbalimbali inayotekelezwa chini ya TACTICS.

Sauti ya Msangi

Naye Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa, Zaina Mlawa, amesema vifaa hivyo vitasaidia Halmashauri kuhakikisha miradi hiyo inatekelezwa kwa ufanisi na kwa kuzingatia viwango vinavyohitajika.

Sauti ya Mlawa