Nuru FM

Manispaa ya Iringa Kuongeza vituo vya kulea watoto mchana

22 September 2026, 11:32

Watekelezaji wa Programu Jumuishi ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto, PJT MMAM. Picha na Adelphina Kutika

Mpango huu unalenga kuwawezesha wazazi kuendelea na shughuli zao za kila siku huku watoto wakiwa katika mazingira salama na yenye huduma za malezi, makuzi, elimu na lishe.

Na Adelphina Kutika

Halmashauri ya Manispaa ya Iringa imeendelea kuimarisha uanzishwaji wa vituo vya kulelea watoto wadogo mchana kupitia Programu Jumuishi ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto, PJT MMAM Lengo likiwa  kuwawezesha wazazi kushiriki katika shughuli za uzalishaji mali bila kuwa na hofu juu ya usalama, malezi na ustawi wa watoto wao.

Haya yanajiri Ndiuka, Kata ya Igumbilo, Manispaa ya Iringa   ambapo  Mkurugenzi wa Halmashauri Ya manispaa Bi Zaina Mlawa ametoa Majengo  Mawili  katika Shule ya Msingi Ndiuka yanatarajiwa kubadilishwa kuwa kituo cha kijamii cha kulelea watoto mchana, kitakachotarajiwa kuhudumia takribani watoto 250.

Sauti ya Wananchi

Wakati wazazi wakieleza umuhimu wa vituo hivyo, Menyekiti wa Soko la Mwamwindi Mlandege Godi Levi Ngahatilwa amesema uanzishwaji wa vituo vya kulelea watoto mchana katika soko  kuta kuwa sehemu muhimu ya kuwalinda watoto wanaoambatana na wazazi wao kwenye shughuli za biashara.

Sauti ya Mwenyekiti

Kwa upande wake, Afisa Ustawi wa Jamii Kanda ya Ruaha  Bi Getrude Tilphone Mbena anaeleza hatua zilizochukuliwa katika uibuaji na uanzishwaji wa vituo vya kijamii, ikiwemo kuwafikia watoto wanaohitaji huduma hizo ni 80  sambamba na kituo cha Matulila Day Care kimefanikiwa kutoa watoto 45 kuanza darasa la awali kati ya watoto 65.

Sauti ya Getrude

Zaina Abas Lehani kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Iringa ameeleza kuwa utekelezaji wa Programu Jumuishi ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto unalenga kuhakikisha kila kata inakuwa na kituo cha kijamii cha kulelea watoto mchana.

Sauti ya Mkurugenzi

Afisa Ustawi wa Jamii Mkoa wa Iringa, Martine Chuwa, amesema kuwa kwa sasa wazazi wameendelea kuonesha mwitikio mkubwa katika uanzishwaji wa vituo vya kulelea watoto mchana, hali inayosaidia kuhakikisha watoto wanapata malezi na uangalizi unaostahili, sambamba na kupunguza vitendo vya ukatili dhidi yao.

Sauti ya Chuwa

Katika Halmashauri ya Manispaa ya Iringa pekee, kuna jumla ya vituo takribani 14 vya kulelea watoto mchana, vinavyolenga kuwapa watoto mazingira salama wakati wazazi wakiendelea na shughuli zao za kila siku.