Nuru FM
22 October 2026, 16:06

Makala hii inaelezea utaratibu unaolenga kuwasaidia Wazee kupata huduma za matibabu bila kubeba gharama zote za matibabu wenyewe.
Na Hafidh Ally
Kwa mujibu wa taarifa ya Wizara ya Afya ya Agosti 2026, Serikali inaendelea kuweka utaratibu wa kugharamia bima kwa wananchi wasio na uwezo. Wazee wenye umri wa zaidi ya miaka 60 wasio na uwezo wanatajwa miongoni mwa makundi yanayostahili huduma za afya zinazogharamiwa na Serikali.