Nuru FM

Maonesho ya Mufindi investment forum and expo yazinduliwa rasmi

17 October 2026, 09:26

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Dkt. Pius Chaya,katiika meza kuu. Picha na Fredrick Siwale

Wawekezaji na wafanyabiashara  wametakiwa kutumia fursa zilizopo katika Wilaya ya Mufindi ili kuchochea ukuaji wa uchumi na kufanikisha utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya Taifa.

Na Fredrick Siwale

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Dkt. Pius Chaya, amezindua rasmi Maonesho ya Mufindi Investment Forum and Expo 2026, yanayofanyika kuanzia Oktoba 16 hadi 20, katika Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa.

Maonesho hayo yanalenga kutangaza fursa za uwekezaji zilizopo Mufindi, kuvutia wawekezaji, kuwaunganisha wafanyabiashara na wadau wa maendeleo pamoja na kuchochea ukuaji wa uchumi wa wilaya hiyo.

Sauti ya Naibu Waziri Chaya

Awali, Mkuu wa Wilaya ya Mufindi, Dkt. Linda Salekwa, amesema maonesho hayo ni jukwaa muhimu la kutangaza fursa za uwekezaji zilizopo katika sekta mbalimbali, zikiwemo kilimo, viwanda, utalii na biashara, huku yakilenga kuwapa wananchi elimu ya namna ya kuzitumia fursa hizo kujiletea maendeleo.

Sauti ya DC Linda

Hata hivyo baadhi ya wadau waliohudhuria maonesho wameonekana kufurahia fursa zinapatikana huku waishukuru Serikali kwa kuandaa maonesho hayo ambayo yamekuwa na chachu kubwa kwao.

Sauti ya Wadau

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Mufindi, George Kavenuke, amesema kongamano hilo ni fursa muhimu ya kuleta mabadiliko ya kiuchumi kwa wananchi wa Mufindi kupitia uwekezaji na biashara.

Jukwaa la Uwekezaji na Maonesho la Mufindi 2026 linafanyika kuanzia Oktoba 16 hadi 20, mjini Mafinga, likilenga kuwakutanisha wawekezaji na wadau mbalimbali ili kutangaza fursa za uwekezaji katika wilaya hiyo, zikiwemo misitu, ufugaji nyuki, utalii ikolojia na biashara ya mazao ya misitu.