Ndejembi aweka jiwe la msingi miradi ya shilingi bilioni 30 MUCE
19 October 2026, 08:59

Miradi hiyo inayofadhiliwa na Serikali kupitia Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET), inalenga kuboresha ufundishaji, ujifunzaji, utafiti na ubunifu katika elimu ya juu nchini.
Na Joyce Buganda
Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Deogratius Ndejembi ameagiza usimamizi madhubuti wa fedha za miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika maeneo mbalimbali nchini ili kuwezesha miradi hiyo kuendana na thamani ya fedha pamoja na ubora
Ndejembi ametoa agizo hilo Mkoani Iringa akiwa katika ziara ya kikazi ya siku moja ambapo ameweka jiwe la msingi katika miradi Saba yenye thamani ya zaidi ya shilingi Bilioni 30 katika chuo kishiriki cha Mkwawa MUCE na kupokea taarifa ya ujenzi wa miradi ya miundo mbinu ya elimu.
Amesema kuwa Miradi hiyo inajumuisha majengo ya sayansi, maabara za kisasa, mabweni ya wanafunzi, maktaba na majengo ya kufundishia.

Naye Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolph Mkenda amesema miradi hiyo inatekelezwa nchini kwa lengo la kuinua elimu ya juu nchini.
Kwa upande wake Mkuu wa Chuo kikuu kishiriki Mkwawa Jakaya Kikwete ametoa neno kwa serikali kuendelea kuboresha chuo hicho kwa kutengeneza miundombinu,Ununuzi wa samani na vifaa vya maabara pia kukamilisha majengo.
Ikumbukwe kuwa Serikali imewekeza zaidi ya trilion 1 katika kuboresha elimu ya juu nchini kupitia mradi wa elimu ya juu kwa mageuzi ya kiuchumi HEET unaotekelezwa kwa kushirikiana na benki ya dunia.
