Nuru FM

Mtatifikolo aridhishwa na ujenzi wa barabara Jimbo la Isiman

13 October 2026, 09:55

Mbunge wa Jimbo la Isiman Emmanuela Mtatifikolo akizungumza na wananchi wa Mahuninga. Picha na Telesia Chalamila

Kukamilika kwa barabara hiyo kumetajwa kuwa chachu katika kurahisisha shughuli za usafirishaji.

Na Telesia Chalamila

Mbunge wa Jimbo la Isimani, Emanuela Mtatifikolo, amefanya ziara ya kukagua miradi ya maendeleo katika Kata ya Mahuninga, huku akiwashukuru wananchi kwa kumchagua kuwa mwakilishi wao.

Akizungumza na wananchi hao, Mtatifikolo amesema ameridhishwa na ujenzi wa barabara ya Iringa Mjini kuelekea Msembe, na kuwataka wananchi kutumia fursa zitakazotokana na barabara hiyo, ikiwemo kuwaandaa vijana kupata elimu ya utalii ili wanufaike na ongezeko la shughuli za utalii.

Sauti ya Mbunge Mtatifikolo

Amesema miradi ya miundombinu inayotekelezwa inalenga kuboresha maisha ya wananchi, kuwawezesha kujikwamua kiuchumi na kuishi katika mazingira salama.

Sauti ya Mbunge Mtatifikolo

Aidha, amewataka wananchi kuchukua tahadhari dhidi ya mvua za El Niño kwa kuepuka maeneo ya mabondeni na kuhifadhi chakula cha kutosha ili kupunguza athari zinazoweza kujitokeza.

Sauti ya Mbunge Mtatifikolo