Nuru FM

Serikali yaanzisha operesheni ya kudhibiti wanyama wakali Iringa

24 September 2026, 09:15

Mkuu wa Mkoa wa Iringa Kheri James akizungumzia kuhusu operesheni ya kudhibiti wanyama wakali. Picha na Chacha Robert

Operesheni hiyo inafanyika kwa ushirikiano wa taasisi mbalimbali ikiwemo TAWA, TANAPA, MBOMIPA, TFS pamoja na vyombo vya ulinzi na usalama, kwa lengo la kuhakikisha wanyama waliotoka kwenye maeneo ya hifadhi wanarejeshwa katika maeneo yao.

Na Chacha Robert

Serikali imeanza operesheni maalumu ya kudhibiti wanyama wakali wanaoingia katika maeneo ya makazi ya wananchi na kusababisha madhara kwa maisha na mali katika baadhi ya maeneo ya Mkoa wa Iringa.

Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Comrade Kheri James, amesema wanyama hao wakiwemo simba, fisi, viboko na tembo wamekuwa wakitoka katika maeneo ya hifadhi na kuingia kwenye vijiji na makazi ya wananchi, hali ambayo imeendelea kusababisha taharuki na madhara kwa wananchi pamoja na mifugo.

Sauti ya Mkuu wa Mkoa

Mkuu huyo wa Mkoa amewataka wananchi kutoa taarifa mapema wanapoona wanyama wakali au makundi ya wanyama yakiingia kwenye vijiji, vitongoji au maeneo ya makazi, huku akisisitiza umuhimu wa kuchukua tahadhari ili kuepusha madhara zaidi.

Sauti ya RC Kheri

Kwa upande wake, Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi, Emmanuel Moirana, amesema vikosi maalumu vimeandaliwa kwa ajili ya kufanya doria pamoja na kuwahamisha wanyama wakali, hususan simba na tembo, huku akisema zoezi hilo ni endelevu.

Sauti ya Kamishna

Naye Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi, Herman Nyanda, amewataka wananchi kutoa taarifa mapema pindi wanapobaini uwepo wa wanyama wakali au waharibifu, akisema mamlaka ziko tayari kupokea taarifa na kuchukua hatua.

Sauti ya Nyanda