Nuru FM

DC Mufindi aitaka NACONGO kuelekeza miradi maeneo yenye uhitaji

22 August 2026, 13:14

Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Linda Salekwa akizungumza katika Jukwaa la Mashirika yasiyo ya Kiserikali. Picha na Hafidh Ally

“Badala ya eneo moja kuwa na miradi ya aina moja inayotekelezwa na mashirika hayo ni vyema wakajigawa na kupeleka miradi hiyo kwenye maeneo yenye uhitaji”

Na Hafidh Ally

Mkuu wa Wilaya ya Mufindi, Dkt. Linda Salekwa, amezitaka taasisi na mashirika yasiyo ya kiserikali yanayotekeleza miradi ya maendeleo wilayani humo kuelekeza nguvu zaidi katika maeneo yenye uhitaji mkubwa wa huduma za kijamii.

Dkt. Salekwa ameyasema hayo wakati wa Jukwaa la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NACONGO) lililofanyika katika Ukumbi wa Mbalamaziwa, Wilaya ya Mufindi. Amesema Serikali inatambua mchango wa mashirika hayo katika maendeleo, hivyo ni muhimu miradi katika sekta za maji, elimu na afya ipelekwe zaidi katika maeneo yenye changamoto.

Sauti DC Linda

Amesema mashirika hayo yamekuwa na mchango mkubwa katika kuisaidia Serikali kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora.

Sauti DC Linda
Ndugu Zacharia Shibukulu kutoka shirika la World Vision akizungumza katika jukwaa la Nacongo.

Kwa upande wake, Zacharia Shibukulu kutoka World Vision Wilaya ya Mufindi, amesema shirika hilo limekuwa likitekeleza miradi katika maeneo yenye uhitaji, ikiwemo afya, elimu, kilimo na ufugaji, hatua iliyowezesha kuwafikia wananchi wengi.

Amesema World Vision kwa sasa inatekeleza shughuli zake katika zaidi ya nchi 100 duniani, ikiwa na lengo la kuchangia upatikanaji wa huduma na maendeleo kwa jamii.

Naye Mwenyekiti wa NACONGO Wilaya ya Mufindi, Phideli Filipatali, amesema umoja huo umejipanga kuendelea kupeleka miradi mbalimbali ya maendeleo kwa wananchi, huku akiunga mkono wito wa Mkuu wa Wilaya wa kuelekeza miradi katika maeneo yenye uhitaji mkubwa.

Mwenyekiti wa NACONGO Wilaya ya Mufindi, Phideli Filipatali akiwa katika jukwaa hilo.

Hata hivyo kupitia jukwaa hilo, baadhi ya wananchi walionufaika na miradi inayotekelezwa na mashirika hayo, walipata fursa ya kujadili namna ya kuongeza mnyororo wa thamani mazao yao sambamba na namna ya kukuza mitaji na kupata masoko