Nuru FM

Kihenzike kuchangia mifuko 200 ya saruji Shule ya Nzivi

19 September 2026, 07:13

Diwani wa Kata ya Mbalamaziwa, Mheshimiwa Aida Kaduma, aliyemwakilisha Mgeni Rasmi, Mheshimiwa David Kihenzile (MB) katika Mahafali. Picha na Fredrick Siwale

Na Fredrick Siwale

Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Mufindi Kusini imeahidi kutoa mifuko 200 ya saruji kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya Shule ya Sekondari Nzivi, iliyopo Wilaya ya Mufindi, Mkoani Iringa.

Ahadi hiyo imetolewa katika mahafali ya 16 ya Shule ya Sekondari Nzivi na Diwani wa Kata ya Mbalamaziwa, Mheshimiwa Aida Kaduma, aliyemwakilisha Mgeni Rasmi, Mheshimiwa David Kihenzile (MB), ambaye ni Mbunge wa Mafinga Kusini na Naibu Waziri wa Ujenzi.

Mheshimiwa Kaduma amesema msaada huo unalenga kuchangia katika kuboresha miundombinu ya shule hiyo kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa elimu.

Sauti ya Kaduma

Akisoma risala mbele ya mgeni rasmi, wanafunzi wa Shule ya Sekondari Nzivi wamesema shule hiyo inakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa mabweni kwa ajili ya wanafunzi wa kike na wa kiume, pamoja na kutokuwa na maktaba.

Sauti ya Mwanafunzi

Naye Katibu wa Umoja wa Wakuu wa Shule za Sekondari Tanzania (TAHOSSA) Wilaya ya Mufindi, Monica Ng’amilo, amesema shule za sekondari zimekuwa zikikabiliwa na ufinyu wa bajeti kwa ajili ya kuendesha shughuli za kila siku.

Amesema baadhi ya changamoto zinazowakabili ni pamoja na ukosefu wa fedha za kugharamia usahihishaji wa mitihani na kuendesha semina za masomo ya kimkakati kwa walimu.

Sauti ya Monica