Kaya tatu Mufindi zapatiwa bima ya afya
10 June 2026, 08:43

Bima hizo zimetolewa ili kuunga mkono juhudi za serikali kuhakikisha jamii inapata huduma bora za afya.
Na Fredrick Siwale
Katika kuunga Mkono upatikanaji wa bima ya afya kwa wote, chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Mufindi kimekabidhi shilingi Sh. 450,000 kwa kaya tatu kwa ajili ya kupatiwa kadi za Bima ya afya.
Akizungumza wakati wa kukabidhi msaaada huo na kutoa elimu ya umuhimu wa Bima ya afya kwa wote katika Zahati ya Changarawe Katibu wa CCM Wilaya ya Mufindi Bw. Clemence Emmanuel Bakuli , amesema Mufindi inaunga mkono juhudi za Rais Dkt. Samia Sululu Hassan kuhusu sera ya afya ili kuboresha ustawi wa jamii.
Awali Mwenyekiti wa CCM tawi la Changarawe Ndg. Hilnedy Aloyce Payovela, ameishauri Serikali kuharakisha uratibu na uhakiki wa huduma za bima ya afya kwa wote huku akiiomba serikali kuweka mchakato vizuri wa utoaji huduma za afya kupitia bima ya afya ili kupunguza changamoto kwa wagonjwa.

Kwa Upande wake Mganga Mfawidhi wa Zahati ya Changarawe Gertrude Emmanuel Liundi , amesema hatua ya Serikali kwa kuanzisha huduma ya bima ya afya kwa wote imesaidia wananchi kupata huduma za afya hasa wakati ambao anakuwa hana fedha kwa wakati huo.
Nao baadhi ya wanufaika wa mpango huo wa bima ya afya kwa wote wameishukuru Serikali na CCM Wilaya ya Mufindi kwa kuwapatia msaada huo jambo litakalosaidia kupata huduma za afya.
Bima ya afya kwa wote ni Mpango huo unaonekana kama hatua muhimu katika juhudi za Serikali za kuhakikisha wananchi wote, hususan wa kipato cha chini, wanapata huduma bora za afya bila kuathiriwa na changamoto za kifedha.