Nuru FM

Mbunge Semuguruka akabidhi matanki ya maji kwa watoto wenye uhitaji Bukoba

22 November 2023, 10:40 am

Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Kagera, Mh Oliver Semuguruka akikabidhi tanki. Picha na Mwandishi wetu.

Na Mwandishi wetu.

Mbunge Oliver Semuguruka afuta machozi ya watoto wenye mahitaji maalum shule ya msingi Mseto Mgeza, Bukoba

Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Kagera, Mh Oliver Semuguruka ametoa msaada wa matanki mawili ya maji yenye ujazo wa lita 5000 kila moja ili kupunguza adha ya maji katika shule hiyo.

Oliver ametoa msaada huo wakati wa mahafali ya shule hiyo iliyopo Bukoba Mjini.

Katika hatua nyingine Mh Oliver ametoa wito kwa wazazi kuacha tabia ya kuwaficha watoto wenye mahitaji maalum.

Amesema watoto wote wanahaki sawa katika nyanja mbalimbali za kimaisha ikiwemo kuwa na haki ya kupata elimu.