Nuru FM

18 Mbaroni Kwa  Wizi  wa Mafuta

9 February 2023, 4:57 pm

Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Iringa ACP Allan  Bukumbi akionyesha baadhi ya madumu yenye mafuta yaliyokamatwa kata ya Ruaha mbuyuni mkoani hapa. Picha na Matukio Daima

Hii ni baada ya oparesheni iliyofanywa na jeshi la polisi mkoani Iringa kuanzia Jan 29 hadi Feb 5 mwaka huu

Na Hawa Mohammed.

Mafuta hayo, mipira 21 ya kunyonyea mafuta kwenye Malori, mapipa nane na chujio sita . Jeshi la Polisi mkoani Iringa Linawashikilia watu 18 akiwemo dereva wa Lori la mafuta (tank) Kwa tuhuma za kujihusisha na biashara ya mafuta ya Dizel na Petrol wanayodaiwa kuyapata kwa njia ya wizi.

Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa polisi mkoani Iringa ACP. Allan  Bukumbi amesema watuhumiwa hao wamekamatwa kufuatia oparesheni maalum iliyofanyika na kukutwa na madumu 158 ya mafuta aina ya Dizel Lita 482 na madumu matupu 305, piki piki mbili ambazo zilikuwa zikitumika kusafirisha

ACP.Allan Bukumbi akieleza mafanikio ya operesheni hiyo

Aidha Kamanda Bukumbi amefafanua  kuwa  mbinu zinazotumiwa na wahalifu hao ni kuiba mafuta kwenye magari mbalimbali yanayoegeshwa pembezoni mwa barabara kuu ya Iringa – Morogoro, na wamekuwa wakishirikiana na  Baadhi ya madereva wa magari ya kubebea mafuta kutoka makampuni  mbalimbali kufanikisha wizi huo Kwa kunyonya  mafuta na kuhamishia kwenye madumu yenye ujazo wa Lita 20 na kuendelea.

ACP.Allan Bukumbi akieleza aina ya wizi unaofanyika

Hata hivyo  Kamanda wa polisi mkoa wa Iringa amesema watuhumiwa wote watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili na  kutoa onyo Kali kwa wote wanaojihusisha na biashara hiyo huku akiwataka wananchi kuendelea kufichua wahalifu na uhalifu Katika maeneo yao .