Nuru FM

Mbunge Ritta Kabati aibana serikali kusambaza Gesi kwa Wananchi

11 May 2023, 11:21 am

Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Iringa Dkt Ritta Kabati akiuliza Swali Bungeni Jijini Dodoma. Picha na Hafidh Ally

Na Hafidh Ally

Mbunge Viti Maalumu Mkoa wa Iringa Dkt Ritta Kabati ameibana serikali kujua mkakati wa kusambaza gesi kwa wananchi wote hapa nchini ili waweze kunufaika na rasilimali hiyo.

Kabati ametoa hoja hiyo katika kipindi cha maswali na majibu ya papo kwa papo Bungeni Jijini Dodoma kwa Waziri Mkuu wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim majaliwa na kuongeza kuwa ni vyema gesi hiyo ikasambazwa kwani Tanzania ni nchi ya kwanza afrika mashariki kutumia Gesi asilia.

Sauti ya Ritta Kabati

Akijibu swali hiilo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amebainisha kuwa ni kweli Tanzania ina gesi asilia na wizara ya Nishati imeweka utaratibu mzuri wa kupanua wigo wa matumizi yake kwa wananchi.

Sauti ya Waziri Majaliwa

Aidha Mh. Majaliwa amebainisha kuwa tayari serikali imeshatangaza zabuni na wameshafungua fursa kwa sekta binafsi kushiriki katika usambazaji wa huduma hiyo ya gesi.

MWISHO