Nuru FM

Mwanahabari Rashid Msigwa Afariki Dunia katika ajali Eneo la ipogolo

19 April 2023, 1:18 pm

Kamanda Mkoa wa Iringa ACP ALLAN BUKUMBI akizungumzia Ajali iliyochukua uhai wa mwanahabari Rashid Maigwa.

Ajali iliyotokea usiku wa kuamkia Leo imeua Mwanahabari na kumjeruhi mwendesha pikipiki eneo la ipogolo Mkoani Iringa.

Na Mwandishi wetu

Mwanahabari Rashid Msigwa Mkazi wa Igumbilo Manispaa ya Iringa amefariki katika ajali iliyotokea eneo la Ipogolo usiku wa kuamkia leo.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa ACP Allan Bukumbi amesema kuwa Msigwa amefariki baada ya gari kupoteza mwelekeo na kugonga bango la hifadhi ya barabara na Mti.

Kamanda Kubumbi akizungumza ajali

Aidha kamanda Bukumbi amesema kuwa ajali hiyo imesababisha majeruhi kwa kijana Joel Mbidula Mkazi wa Ipogolo aliyekuwa dereva wa pikipiki akitoka Ipogolo.

Gari aliyokuwa akiendesha Marehem Rashi d Msigwa baada ya Ajali.

Katika tukio lingine Kamanda Bukumbi amesema kuwa kuna wachimbaji  4 wamefariki dunia na wengine watatu wameokolea katika mgodi wa Igoma Kata ya sadan wilaya ya Mufindi baada ya kufukiwa na kifusi kilichosabishwa na mvua kunyesha.

Sauti ya Kamanda