Nuru FM

Mapesa awaagiza maafisa kilimo Idodi mashine za kukoboa mpunga

8 April 2024, 9:01 am

Afisa Tarafa ya Idodi Mapesa Makala akitoa maagizo kwa maafisa kilimo. Picha na Joyce Buganda

Na Joyce Buganda

Maafisa kilimo wa Tarafa ya Idodi iliyopo wilaya ya Iringa wameagizwa kutafuta mashine za kukoboa mpunga na kuzipeleka katika eneo hilo ili kumpunguzia mkulima gharama za usafirishaji wa zao hilo mpaka Iringa mjini.

Hayo yamezungumzwa  na Afisa Tarafa wa  ya idodi Makala Mapesa wakati akizungumza na wananchi ikiwa ni mara ya kwanza kufika eneo hilo la kazi siku chache baada ya kuteuliwa katika nafasi hiyo ambapo amefafanua kuwa eneo la Idodi lina wakulima wa mpunga wengi lakini wanakumbana na changamoto ya kusafiri umbali mrefu kwenda kukoboa zao hilo.

Sauti ya Mapesa

Aidha Mapesa amewasihi wakazi wa eneo hilo walime kisasa ili kupata mazao yenye tija yatakayochochea watu wa nje kuifahamu Tarafa hiyo kupitia kilimo.

Sauti ya Mapesa

Kwa upande wao baadhi ya Wananchi wa vijiji vya Tarafa ya Idodi wamepongeza kauli ya Afisa huyo ya kuletwa mashine za kukoboa mpunga kwani kutawaepushia gharama za kufanya kilimo  na kuongeza ushindani wa kibiashara.

.

MWISHO