Nuru FM

Fettilicious Kiboko ya Vitambi awataka vijana kutokata Tamaa ya kufanya biashara Mtandaoni

7 February 2023, 7:33 pm

Mfanyabiashara wa Bidhaa za Vipodozi na Bidhaa ya kupunguza Mwili maarufu Fettilicious Kiboko ya Vitambi.

Ni vyema Mfanyabiashara wa biashara za Mtandaoni ukawa na lugha nzuri kwa wateja wako ili kuongeza wigo wa wateja wapya.

Na Ansigary Kimendo

Vijana na wanawake wajasiriamali Manispaa ya Iringa wametakiwa kutohofia kutangaza biashara zao kupitia Mitandao ya Kijamii kwani dunia imehamia Kiganjani.

Akizungumza na Nuru FM ofisini kwake, Fetty  maarufu kwa jina la Fettilicous Kiboko ya Vitambi ambaye amekuwa akitumia mitandao ya kijamii kutangaza biashara zake za dawa za mitishamba na bidhaa za vipodozi amesema kuwa kikubwa unatakiwa kuwa muaminifu pindi unapofanya biashara hiyo ili uweze kuwapata wateja ambao itakulazimu uwatumie bidhaa zao.

Fetty akizungumzia kuhusu faida za kutangaza biashara Mtandaoni

Fetty ambaye amejizolea umaarufu kwa dawa yake ya Kiboko ya Vitambi ambayo inapunguza Mwili na nyama za tumboni bila madhara yoyote amesema kuwa dawa zake hazina kemikali jambo lililopelekea wateja wake kumuamini.

“Kwa kweli mimi dawa zangu hazina madhara, na jinsi nnavyowatangazia watu kupitia ukurasa wangu wa instagram wa @Fettiliciou_kiboko_ya_vitambi na Mtandao ya watu maarufu hapa nchini, imepelekea wateja wangu waniamini na kwa sasa wanaweza kuagiza mzigo kwangu na nikawatumia popote walipo na hata nje ya Nchi pia ninatuma bidhaa zangu. Kwa ambao wanataka bidhaa zangu wanaweza kunipigia kwa simu namba 0764-453454” alisema Fetty

Fetty ambaye ni Mwanamke mwenye bashasha Muda wote amesema kuwa ni vyema ukawa na lugha nzuri kwa wateja wako ili kuongeza wigo wa wateja wapya huku akizungumzia mafanikio aliyoyapata kutokana na shughuli hiyo ni pamoja na kuwa na marafiki wengi na kupata fedha za kuendesha familia.

Amesema kuwa mara ya kwanza kuingia katika biashara ya kutangaza Mtandaoni alikuwa na hofu baada ya kukutana na matapeli ambao wamekuwa wakitumia jina lake vibaya huku baadhi ya wadukuzi wa mtandao wakitaka kuiba Acount za Mitandao yake, ila aliweza kukabiliana na vikwazo hivyo na kufikia malengo yake.