Nuru FM

Rais Samia atangaza kifo cha Mwinyi

29 February 2024, 9:26 pm

Rais Mstaafu Ally Hassan Mwinyi amefariki Dunia.

Na Mwandishi wetu.

Rais Mstaafu wa awamu ya pili wa Tanzania, Ally Hassan Mwinyi amefariki dunia leo Februari, 2024 saa 11:30 jioni katika hospitaliya Mzena jijini Dar es Salaam alipokuwa akipatiwa matibabu ya ugonjwa wa saratani ya mapafu.

Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ametangaza msiba huo leo ambapo amesema mzee Mwinyi alikuwa akipatiwa matibabu tangu Novemba 2023 London Uingereza na baadaye kurejea nchini na kuendelea na matibabu hospitali ya Mzena.

Rais Samia ametangaza siku saba za maombolezo kuanzia kesho kufuatia kifo hicho.