Nuru FM

CCM Mufindi yahimiza uwajibikaji kwa miradi ya maendeleo

2 February 2026, 11:39

Picha ya Viongozi wa CCM Wilaya ya Mufindi wakiongozwa na Mwenyekiti George Kavenuke. Picha na Fredrick Siwale

Na Fredrick Siwale

Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Mufindi kimeanza kutoa elimu ya uwajibikaji kwa viongozi wake kuanzia ngazi ya Matawi ili kuleta maendeleo kwa jamii.

Hayo yamezungumzwa na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa George Kavenuke, wakati wa kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya na kuongeza kuwa hatua hiyo itasaidia kuongeza morali kwa watendaji kufanya kazi kwa bidii.

Sauti ya Kavenuke

“Tayari tumeshaanza kutembelea, Mabarozi, Mashina, Matawi, Kata na Wilaya kufanya amsha amsha na kuwasha moto wa kufanyakazi na kuwajibika kwa vitendo” Alisema Kavenuke. 

Akichangia katika kikao hicho Mbunge wa Mufindi Kusini na Naibu Waziri wa Uchukuzi Mh. David Kihenzile amesema ni wakati wa kusimamia ilani ya chama kwa kuhakikisha wanaharakisha ujenzi wa barabara za wilaya hiyo.

Sauti ya Mbunge Kihenzile

Naye Mbunge wa Jimbo la Mufindi Kaskazini Exaud Kigahe amesema umefika wakati wa kuunganisha nguvu kwa pamoja ili kuhakisha  miundo mbinu ya barabara inatengemaa hasa mafinga-mgololo na mafinga madibila ambazo zimekuwa kero kwa wananchi.

Sauti ya Mbunge Kigahe

“Mimi na Waheshimiwa Wabunge wenzangu Mufindi Kaskazini, Mufindi Kusini na Mafinga Mjini tutahakikisha tunaweka kipaumbele katika barabara za Nyigo- Mgololo  Mafinga – Madibila na  Mafinga  kwenda Mlimba” Alisema Mh. Kigahe. 

Awali Mbunge wa Viti Maalumu kupitia Vijana Mh. Jasmine Ng’umbi na Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Iringa Agrey Tonga wameomba vijana kuwa na uzalendo pale wanapotimiza majukumu yao.

Sauti ya Tonga na Jasmine