Mwang’onda: “Tuilinde amani ya nchi”
28 May 2026, 08:55

Na Fredrick Siwale
Wananchi Halmashauri ya Mji Mafinga Mkoani Iringa wametakiwa wametakiwa kulinda amani iliyopo Nchini kwani ndio msingi wa kutekeleza miradi mikubwa ya maendeleo.
Akizungumza katika mkesha wa Mwenge uliofanyika Uwanja wa Shule ya Msingi Mkombwe Halmashauri ya Mji Mafinga Kiongozi wa mbio za Mwenge wa uhuru Kitaifa, Ndugu Wazo Mwang’onda amesema kuwa amani ni tunu ya Taifa huku akizitaka Taasisi zote kuhubiri faida za amani.
Aidha Mwang’onda amewataka wazazi kuwafundisha vijana wao kuwa na maadiili mema sambamba na kujilinda na maambukizi ya Ukimwi na matumizi ya dawa za kulevya hasa vijana walio katika rika la balehe.
“Vijana wenye umri wa kuanzia miaka 15-24 wako katika hatari ya kupata maambukizi ya Ukimwi hivyo wazazi wanapaswa kuchukua hatua za kuwalinda na janga hili” Alisema Wazo

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Mafinga Mjini Mh. Dickson Lutevele VILLA amesema kuwa wamepokea maagizo ya Kiongozi wa mwenge kwa kuwa wanashirikiana na viongozi wote wa Halmashauri ili kusimamia miradi ya maendeleo.
Awali Mbunge wa Vitimaalum kupitia Vijana Mh. Jasmine Ng’ombi ameishukuru Serikali chini ya Uongozi wa Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha kwa ajili ya miradi ya Maendeleo iliyotekelezwa kwa wakati katika jamii.
