Nuru FM

Miaka mitatu ya Rais Samia yainufaisha hospitali ya Rufaa Iringa

25 March 2024, 10:19 am

Mganga Mfawidhi wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Iringa Dkt.Afred Mwakalebela akizungumzia mafanikio ya sekta ya afya katika hositali ya rufaa ya Iringa. Picha na Ayoub Emanuel

Katika kipindi cha miaka 3 ya Uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Iringa ilipokea shilingi billion 4.4 kwaajili ya kuboresha huduma za afya ndani ya hospitali hiyo.

Na Hafidh Ally

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa WA Iringa Dkt.Afred Mwakalebela amesema katika kipindi cha miaka 3 ya Mh Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Iringa imefanikiwa kuboresha huduma za afya.

Akizungumza na Nuru fm, Dkt. Mwakalebela amesema kuwa maboresho makubwa yaliyofanyika na Serikali kupitia wizara ya afya ni pamoja na ujenzi wa jengo la radiolojia na ununuzi wa mashine ya CT SCAN na digital X_RAY umesaidia wakazi wa mkoa wa Iringa kutofata huduma hiyo katika Mikoa ya Dodoma na Dar Es Salaam.

SAUTI YA MWAKALEBELA

Akiendelea kutaja maboresho yaliyofanyika ndani ya kipindi cha miaka 3 ya Mh.Rais amesema kuna vifaa tiba aina ya ECG ambavyo vimenunuliwa katika hospitali hiyo ili kuangalia shida ya moyo  wagonjwa sambamba na ujenzi na vifaa katika jengo la dharura ambapo lina uwezo wa kuhudumia wagonjwa Zaid ya 50.

SAUTI YA MWAKALEBELA

Mfawidhi huyo amesema ndani ya hospitali hiyo kwasasa Kuna kitengo cha kuchuja damu(Dialysis) ambapo hapo awali wagonjwa Hao walilazimika kuhama maeneo wanayooishi ili kufata huduma hiyo Dodoma lakini ndani ya miaka 3 ya Mh.Rais kitengo hicho kimepatikana.

Akitaja maboresho mengine amesema ni uwepo wa kitengo cha viungo bandia ambacho kimejengwa na wadau ambao ni Mnec wa Mkoa WA Iringa Ndugu Salim Abri Asan pamoja na VICENZA.

Sambamba na hayo ni uwepo wa wodi ya wagonjwa mahututi yenye vitanda 16 pamoja na mashine zake,na Jengo la V.I.P ambapo amesema jengo la hilo la VI.P pia limejengwa na ndugu Salim Abri Asas.