Nuru FM

Fisi wajeruhi mifugo Mufindi- Wananchi kuchukua tahadhari

6 July 2023, 10:34 am

Mnyama wa Porini Fisi. Picha kwa msaada wa Mtandao

Na Mwandishi

Wananchi wilayani Mufindi wametakiwa kutoa ushirikiano wa kumsaka fisi ambaye ameua mifugo aina ya Nguruwe wawili kondoo Wanne na kujeruhi kuku katika bonde la Mgololo.

Akitoa ufafanuzi wa sintofahamu iliyozuka katika kata ya Makungu, Afisa Habari na Mawasiliano Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi Bw. Ndimyake Mwakapiso, amesema baada taharuki kuwakumba wananchi wa kijiji cha Mabaoni na Lole wakihofia kuwa ni Simba kufuatia uchunguzi uliyofanywa na Afisa Wanyamapori umebaini kuwa ni Fisi.

Mwakapiso amewataka wananchi kuishi kwa tahadhari wakati juhudi za kumtafuta na kumuuwa mnyama huyo zikiendelea.

Awali Kaimu Mwenyekiti wa kamati ya Ulinzi na Usalama Kijiji Cha Mabaoni Ndg Thobias Jonas Mkwama amethibitisha kupata taarifa hizo toka kwa mmiliki wa Mifugo Ndg Amlike na hatua zikachukuliwa kwenda eneo la Tukio kuona Hali halisi.

Afisa Mifugo kata ya Makungu Ndg Evaldo Mavika amesema baada ya kufika eneo la Tukio walifuatilia alama za nyanyo za mnyama huyo na kukuta zikiwa zimesalia kilogram 3 pekee za nyama.