Nuru FM

UWT Iringa watoa msaada Zahanati ya Kising’a

23 March 2024, 11:38 am

Mwenyekiti wa UWT Iringa vijijini Lena Hongole akizungumza baada ya kukabidhi msaada katika Zahanati ya Kising’a. Picha na Ayoub Emanuel.

Licha zahanati Kising’a kutoa huduma za kitatibu bado Kuna changamoto ya upungufu wa vifaa tiba.

Na Fabiola Bosco

Umoja wa wanawake wa Chama cha Mapinduzi wilaya ya Iringa umekabidhi mablanketi 16 na vifaa vya usafi katika zahanati ya kising’a  yaliyotolewa na Rais Samia Suluhu Hassan

Kwa mujibu wa Lena Hongole amesema vifaa hivyo vitakuwa msaada kwa zahanati kwani zimekuwa zikipitia changamoto ya ukosaji wa vifaa tiba.

Sauti ya UWT

Amesema vifaa hivyo vitumike kama ilivyotakiwa kwani mahitaji ni makubwa huku akiahidi kufikisha vifaa vingine vitakavyotolewa na waheshimiwa wabunge.

Sauti ya UWT