Nuru FM

CCM Iringa Yatekeleza miradi ya afya na kilimo

22 March 2023, 9:22 am

Mwenyekiti wa CCM Iringa Daud Yassin akizungumzia Miradi ya maendeleo Iringa- Picha na Mwandishi wetu

Miradi inayotekelezwa Mkoani Iringa na serikali ni pamoja na miradi ya afya na Kilimo.

Na Adelphina Kutika

Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa Iringa kimeendelea kutekeleza miradi ya maendeleo nchini ikiwemo sekta ya afya na kilimo.

Kwa mujibu wa  Mwenyekiti  wa CCM  Mkoa wa Iringa Daudi Yasini,  serikali ya awamu ya sita imefanikiwa kuboresha  Ujenzi wa vituo vya  afya, hospital za wilaya,  na  za Rufaa

Sauti ya Mwenyekiti wa CCM iringa akizungumzia miradi ya maendeleo

“Mbali na sekta ya afya serikali  Sserikali imeongeza upatikanaji wa pembejeo za kilimo” alisema Yassin.

Baadhi ya viongozi wa serikali na taasisi binafsi wameeleza hisia zao juu ya uongozi huo mahiri wa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kipindi cha miaka miwili.

Sauti ya Viongozi wa serikali na taasisi binafsi wakizungumzia miaka miwili ya Rais Samia

Wakizungumzia kupungua kwa gharama za pembejeo za kilimo baadhi ya wananchi  katika  manispaa ya Iringa wameeleza  namna ilivyowapunguzia makali ya maisha .

Hayo yanajiri wakati Tanzania ikiadhimisha miaka miwili ya rais samia suluhu madarakani baada ya mtangulizi wake Hayati Dr John Pombe Magufuli.

MWISHO.